-
Mashirika ya haki za binadamu yatahadharisha kuhusu amri ya Trump ya kuwazuia Waislamu kuingia Marekani
Jan 26, 2025 03:37Wanaharakati wa haki za kiraia wameitaja amri mpya ya kiutendaji iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani inayowazuia raia wa nchi za Kiislamu kuingia Marekani kuwa ina taathira kubwa zaidi kuliko kile kilichoshuhudiwa mwaka 2017 na katika awamu ya kwanza ya serikali yake.
-
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kazan: Kifarsi, ni lugha ya pili ya Waislamu nchini Russia
Jan 26, 2025 03:34Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kazan huko Russia amesema kuwa Kifarsi ni lugha ya pili inayotumiwa na Waislamu nchini humo.
-
Masomo ya watoto milioni 240 yalivurugwa na hali mbaya ya hewa 2024
Jan 25, 2025 07:50Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umesema ratiba ya masomo ya takriban wanafunzi milioni 242 katika nchi 85 duniani yalitatizwa na hali mbaya ya hewa mwaka 2024.
-
Russia: Kwa mtazamo wa mkuu wa UNICEF watoto wa Ghaza si muhimu kama wenzao wa Ukraine
Jan 25, 2025 02:42Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amemshutumu mkuu wa UNICEF kwa kuwapa kipaumbele watoto wa Ukraine kuliko watoto wenzao wa Ghaza baada ya kushindwa kulieleza Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu masaibu ya watoto hao kama alivyofanya kwa watoto wa Ukraine.
-
Marekani yasimamisha misaada mipya ya fedha nje ya nchi, Israel na Misri hazimo
Jan 25, 2025 02:42Serikali mpya ya Marekani imetangaza kuwa inasitisha takribani ufadhili wote mpya wa msaada wa fedha wa nje ya nchi isipokuwa kwa washirika wake wawili ambao ni utawala wa Kizayuni wa Israel na Misri. Haijafahamika wazi kama uamuzi huo utaihusu pia Ukraine au la.
-
Changamoto zinazoikabili Ulaya mbele ya Sera za Trump: Wasiwasi na wahka
Jan 24, 2025 23:30Wakati Donald Trump akianza muhula wake wa pili kama Rais wa Marekani, nchi za Ulaya zimeingiwa na wasiwasi na wahka mkubwa kuhusu sera zake. Sasa, maafisa wa nchi za Ulaya wanatafuta njia za kushughulikia changamoto zinazojitokeza baina pande hizo mbili, kuanzia kwenye vitisho vya kibiashara hadi masuala ya usalama.
-
Trump: Dola bilioni 600 inazotaka Saudia kuwezeka Marekani hazitoshi
Jan 24, 2025 23:27Rais Donald Trump ametoa wito kwa Saudi Arabia kuongeza kiwango cha uwekezaji wake nchini Marekani hadi dola trilioni moja.
-
Ujio wa Trump; Marekani yawakamata na kuwafukuza mamia ya wahamiaji
Jan 24, 2025 23:26Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House ya Marekani amefichua kuwa, katika wiki ya kwanza ya urais wa Donald Trump, wahamiaji haramu 538 wamekamatwa na kuzuiliwa, huku mamia ya wengine wakifukuzwa nchini.
-
Watoto wenye matatizo ya afya ya akili wazidi kuongezeka nchini Uingereza
Jan 24, 2025 03:27Idadi ya watoto wanaokabiliwa na matatizo ya afya ya akili nchini Uingereza inaripotiwa kuongezeka na kuibua wasiwasi mkubwa katika jamii ya hiyo ya bara Ulaya.
-
Moscow: Marekani inachuma pesa kutokana na vita vya Ukraine
Jan 24, 2025 00:04Msemaji wa Kremlin amekosoa himaya ya kifedha na kisiasa ya Washington kwa serikali ya Kiev na kusema: Marekani inapata pesa kwa kuuza rasilimali zake za nishati za bei ya juu kwa watu wa Ulaya walioathiriwa na vita.