-
Putin amwambia Merkel: Nisamehe, sikujua kuwa unaogopa mbwa
Nov 30, 2024 07:51Rais wa Russia, Vladimir Putin, amemuomba radhi Kansela wa zamani wa Ujerumani, Angela Merkel, akisisitiza kwamba hakumtisha kwa makusudi alipomuingiza mbwa wake katika mkutano waliofanya mwaka 2007, baada ya Merkel kuandika tukio hilo katika kitabu cha kumbukumbu zake kilichochapishwa hivi majuzi.
-
Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN: Miezi 13 ya vita imeifanya Ghaza kuwa jehanamu
Nov 30, 2024 03:39Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ofisi ya Ukanda wa Ghaza (OHCHR) unaokaliwa kwa mabavu Ajith Sunghay amesema miezi 13 ya vita imeufanya Ukanda huo kuwa kama jehanamu, kwani kuna uharibifu usio na kifani, njaa isiyoelezeka, maradhi na mwendelezo wa mashambulizi ya mabomu yanayowatawanya raia kila uchao.
-
Borrell: Misimamo ya EU kuhusu vita vya Ghaza na Ukraine imeonekana kuwa ya undumilakuwili
Nov 30, 2024 02:35Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya anayemaliza muda wake amekiri kuwa umoja huo umekuwa na "undumilakuwili" katika misimamo yake isiyo namna moja kuhusiana na vita vya Ukraine na Ghaza na kubainisha kwamba hisia hizo zimekuwepo sana katika nchi za Kusini mwa Ulimwengu.
-
Mkuu wa Mashtaka wa ICC: Rufaa ya Israel ya kupinga hati ya kukamatwa Netanyahu itupiliwe mbali
Nov 30, 2024 02:33Karim Khan, Mkuu wa Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amesema rufaa iliyokatwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya hati za kukamatwa waziri mkuu wake Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa vita Yoav Gallant inapasa zitupiliwe mbali.
-
Vyombo vya habari vya Magharibi vyakosolewa kwa kuipendelea Israel licha ya kufanya mauaji ya kimbari Gaza
Nov 29, 2024 23:27Licha ya hali mbaya ya hewa, mamia ya waandamanaji wamekusanyika nje ya Ukumbi wa Jiji la Belfast kueleza wasiwasi wao kuhusiana na upendeleo wa vyombo vya habari vya nchi za Magharibi kwa utawala wa kizayuni wa Israel, licha ya utawala huo kuendelea kufanya mauaji ya kimbari huko Palestina
-
Australia yaweka historia, yapitisha sheria ya marufuku kwa watoto kutumia mitandao ya kijamii
Nov 29, 2024 23:18Seneti ya Australia imepitisha sheria za kupiga marufuku watoto na vijana wadogo kutumia mitandao ya kijamii, ukiwa ni uamuzi wa kwanza wa aina yake kuchukuliwa na serikali yoyote ulimwenguni.
-
Ombi la kukamatwa kiongozi wa kijeshi wa Myanmar
Nov 29, 2024 23:05Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) amemshutumu kiongozi wa kijeshi wa Myanmar kwa kufanya jinai dhidi ya binadamu katika kuwakandamiza Waislamu walio wachache wa Rohingya.
-
Mienendo ya kindumakuwili ya Ulaya kuhusu waranti ya kukamatwa watawala wa Israel
Nov 29, 2024 11:57Hatua ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ya kutoa waranti ya kukamatwa Benjamin Netanyahu na Yoav Gallant, Waziri Mkuu na waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel imeakisiwa pakubwa kimataifa kwa kutilia maanani umuhimu wake na pia kutokana na kutochukuliwa hatua kama hiyo huko nyuma dhidi ya viongozi wa utawala huo ghasibu.
-
Russia: Marekani na Uingereza zinaeneza machafuko ndani ya Syria kupitia magenge ya kigaidi
Nov 29, 2024 08:11Russia imesema madola makubwa ya Magharibi yanayoongozwa na Marekani yanaendelea na vitendo vyao vya chuki dhidi ya Syria kwa kuwaunga mkono wanamgambo wanaoipinga serikali ya Damascus pamoja na makundi ya kigaidi ya kitakfiri katika kila pembe ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
UK: Tutamtia mbaroni Netanyahu akikanyaga ardhi ya Uingereeza
Nov 28, 2024 23:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amedai kuwa nchi yake inaheshimu uamumizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kutiwa mbaroni waziri mkuu wa Israel, Banjamin Netanyahu na kusisitiza kuwa, kama Netanyahu atakanyaga ardhi ya Uingereza, basi London itamtia mbaroni.