UK: Tutamtia mbaroni Netanyahu akikanyaga ardhi ya Uingereeza
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amedai kuwa nchi yake inaheshimu uamumizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kutiwa mbaroni waziri mkuu wa Israel, Banjamin Netanyahu na kusisitiza kuwa, kama Netanyahu atakanyaga ardhi ya Uingereza, basi London itamtia mbaroni.
Shirika la habari la Mehr limemnukuu David Lindon Lammy akitoa madai hayo bila ya kulaani wala kuashiria jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni na kusema kuwa ba Uingereza inaheshimu uamuzi wa Mahakama ya ICC dhidi ya Netanyahu na kwamba hakuna kitu chochote kitakachoizuia London kutekeleza hukumu hiyo.
Vilevile amesema kuwa mazungumzo yanaendelea kati yake na wakuu wa utawala wa Kizayuni kuhusu masuala yaliyobakia yanayohusiana na kusimamishwa vita Ukanda wa Ghaza na wajibu wa kuruhusiwa mashirika mbalimbali kuwafikishia misaada wakazi wa ukanda huo.
Alkhamisi ya tarehe 21 Novemba 2024, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilitoa waranti wa kutiwa mbaroni waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na waziri wake wa zamani wa vita, Yoav Gallant, kutokana na jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza zikiongozwa na viongozi hao wawili wa Israel.
Baada ya kutolewa hukumu hiyo, nchi nyingi duniani hata za Ulaya na Amerika zimetangaza kuwa zitaheshimu uamuzi huo wa Mahakama ya ICC kiasi kwamba hata Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell amesema kuwa umoja huo utaheshimu na kutekeleza kivitendo hukumu hiyo dhidi ya Netanyahu na Galland.