-
CAIR yamjibu Papa: Mauaji ya kimbari ya Ghaza si ya kuchunguzwa, ni jambo lililo dhahiri
Nov 18, 2024 03:11Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limekaribisha wito wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis wa kufanywa uchunguzi ili kubaini kama utawala wa Kizayuni umefanya mauaji ya kimbari ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, lakini limesisitiza kuwa hauhitajiki uchunguzi na uthibitisho kwa jambo lililo dhahiri.
-
Uhispania yasisitiza kusimamishwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza na Lebanon
Nov 18, 2024 03:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania amesisitiza ulazima wa kusitishwa haraka iwezekanavyo mashambulizi ya kikatili yanayofanywa na jeshi la Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
-
Biden aidhinisha Ukraine kutumia makombora ya US kushambulia ndani ya ardhi ya Russia
Nov 18, 2024 03:09Rais Joe Biden wa Marekani ameripotiwa kuidhinisha Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu ya Kimarekani kulenga shabaha ndani ya mipaka ya Russia ya kabla ya 2014. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya jana Jumapili iliyotolewa na gazeti la New York Times likiwanukuu maafisa wa Marekani ambao hawakutaka kutajwa majina yao.
-
Waungaji mkono wa Palestina waandamana Canada na kulaani jinai za Israel
Nov 17, 2024 23:06Mamia ya raia nchini Canada wameandamana katika mji mkuu Ottawa na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na kulaani mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza.
-
China yaibainishia Marekani mistari yake minne myekundu ambayo haipasi kuvukwa
Nov 17, 2024 23:06Rais Xi Jinping wa China ameweka wazi mistari myekundu minne ambayo amesema haipasi kuvukwa na Marekani ili kuwepo uhusiano wenye usawa na sahihi kati ya nchi hizo mbili.
-
Kuongezeka kwa maandamano barani Ulaya dhidi ya jinai za Wazayuni
Nov 17, 2024 08:51Kuendelea kwa jinai za Wazayuni katika Ukanda wa Gaza na Lebanon kumepelekea kupanuka uungaji mkono kwa Palestina na chuki dhidi ya Wazayuni barani Ulaya.
-
Mabinti wa Malcolm X waishtaki Polisi, FBI na CIA kwa kumuua baba yao 'kwa kukusudia'
Nov 17, 2024 08:32Mabinti wa Malcolm X wamechukua hatua za kisheria za kulishtaki jeshi la Polisi la Marekani, Polisi ya Upelelezi (FBI) na Shirika la Ujasusi la nchi hiyo (CIA) kwa kumuua baba yao kwa "kukusudia".
-
Euro-Med Human Rights Monitor: Israel inanyonga raia wa kaskazini mwa Gaza
Nov 17, 2024 04:20Shirika la kutetea haki za binadamu la Euro-Med limesema kwamba limesajili makumi ya kesi za mauaji ya kukusudia na vitendo vya kunyongwa raia vinavyofanywa na jeshi la Israel Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, ndani ya mfumo wa mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina yanayoendelea kwa zaidi ya miezi 13.
-
Ripota wa Umoja wa Mataifa aishutumu Uingereza kwa kukana mauaji ya kimbari huko Gaza
Nov 16, 2024 22:58Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amekosoa matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuhusu mauaji ya kimbari yanayofanyika huko Gaza na kusema kwamba anakanusha kutokea jinai hiyo katika eneo hilo la Palestina.
-
'Nelson Mandela Mwarabu' aachiwa huru baada ya kufungwa jela miaka 40 nchini Ufaransa
Nov 16, 2024 22:56Mahakama ya Ufaransa imeamuru kuachiliwa kwa mwanamapambano wa Lebanon, Georges Ibrahim Abdallah, ambaye alikamatwa miaka 40 iliyopita kutokana na mauaji ya maajenti wa Marekani na Israel mjini Paris.