-
Slovenia yaitambua rasmi nchi huru ya Palestina
Sep 26, 2024 03:14Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Waziri Mkuu wa Slovenia Tanja Fajon ametangaza kuwa nchi hiyo imeitambua rasmi nchi huru ya Palestina.
-
Putin aamuru mwongozo wa utumiaji silaha za nyuklia wa Russia ufanyiwe mabadiliko
Sep 26, 2024 01:39Rais Vladimir Putin wa Russia ameamuru mwongozo wa utumiaji silaha za nyuklia wa nchi hiyo ufanyiwe mabadiliko akionya pia kuwa nchi yake inaweza kujibu mapigo kwa silaha za nyuklia ikiwa itashambuliwa kwa silaha za kawaida zilizotolewa na dola linalomiliki silaha hizo.
-
Tuhuma na misimamo ya kurudiwarudiwa ya Marekani kwa ulimi wa Joe Biden katika Umoja wa Mataifa
Sep 26, 2024 00:28Jumanne ya wiki hii, rais wa Marekani, Joe Biden, alitoa hotuba yake ya mwisho katika kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kukariri madai ya uongo ya siku zote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na dhidi ya kambi ya Muqawama. Rais wa Marekani alidai kuwa eti serikali yake inapigania kuleta amani na utulivu katika ukanda wa Asia Magharibi.
-
Trump: Mashariki ya Kati inalipuka, tunaelekea kwenye Vita vya Tatu vya Dunia
Sep 25, 2024 04:28Mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa dunia inaweza kuwa katika ncha ya Vita vya Tatu vya Dunia, akionya juu ya mlipuko wa Mashariki ya Kati. Trump pia ameishutumu Washington kuwa imeshindwa kushughulikia migogoro hiyo.
-
Russia yatahadharisha kuhusu athari za matukio ya karibuni huko Lebanon
Sep 24, 2024 22:58Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu matokeo ya matukio ya karibuni huko Lebanon katika mfumo wa kimataifa.
-
Profesa Fraihat: Vita vya Lebanon ni vya tatu vinavyofadhiliwa na serikali ya Biden
Sep 24, 2024 07:36Ibrahim Fraihat, Profesa wa Taaluma ya Usuluhishi wa Mizozo ya Kimataifa katika Taasisi ya Doha ya Mafunzo ya Wahitimu, amesema kupanuka kwa vita vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza hadi Lebanon kulitarajiwa, lakini kile ambacho hakikutarajiwa ni idadi kubwa ya vifo ndani ya muda wa siku moja.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza: Vita vya Ukraine vinaweza vikavuka mwaka 2026
Sep 24, 2024 07:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy ametabiri kuwa mapigano kati ya Russia na Ukraine huenda yakaendelea kwa angalau miaka miwili zaidi na kuvuka mwaka 2026.
-
Akthari ya wananchi wa Marekani wanataka nchi yao irejee katika mapatano ya JCPOA
Sep 23, 2024 22:49Watu wengi nchini Marekani wanataka Washington irudi katika Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA). Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika huko Marekani.
-
Rais wa Colombia alaani kimya cha vyombo vya habari kwa mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel Ghaza
Sep 23, 2024 04:24Rais Gustavo Petro wa Colombia amelaani kimya kinachoonyeshwa kwa vita vya kinyama vinavyoendelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, na kusisitiza kwamba mauaji ya kimbari yanafanyika huko Palestina.
-
UN yapitisha Mkataba wa Zama Zijazo (Pact for the Future), Guterres: Sasa ni wakati wa vitendo
Sep 23, 2024 03:39Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha Mkataba wa Zama Zijazo (Pact for the Future) baada ya vuta nikuvute zilizokuwepo ambapo Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres ameshukuru wawezeshaji wote waliojitolea kufanikisha kupitishwa kwa mkataba huo adhimu.