-
Hatua mpya ya Ujerumani dhidi ya Uislamu, kupigwa marufuku kazi za kituo cha Kiislamu
Jul 26, 2024 07:04Serikali ya Ujerumani imepiga marufuku shughuli za kituo cha Kiislamu cha Hamburg na taasisi tanzu za kituo hicho licha ya umuhimu wake mkubwa kwa Waislamu.
-
Kongresi ya Marekani yakosolewa kwa kumpa mhalifu wa kivita jukwaa la kuhutubia
Jul 25, 2024 07:26Kongresi ya Marekani imekosolewa sana kwa kumpa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, jukwaa la kuhutubia wawakilishi na maseneta wa nchi hiyo licha ya kiongozi huyo kutambuliwa kuwa ni mhalifu wa kivita na mtenda jinai dhidi ya binanadamu kutokana na mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza.
-
Rashida Tlaib amkabili Netanyahu katika Bunge la Marekani kwa kumwita "mhalifu wa kivita"
Jul 25, 2024 07:25Mwakilishi wa chama cha Democratic katika Kongresi ya Marekani, Rashida Tlaib amepinga hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, katika Congress jana, Jumatano, na kutaka awajibishwe kwa mauaji ya kimbari yanayofanyika Ukanda wa Gaza.
-
Wito wa kutaka Israel ipigwe marufuku katika michezo ya Olimpiki ya Paris kutokana na jinai za Gaza
Jul 25, 2024 01:05Shirika moja la haki za binadamu lenye makao yake nchini Marekani linasema utawala katili wa Israel unapaswa kuzuiwa kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 kutokana na uamuzi wa hivi majuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu jinai za kinyama za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Ujerumani yapiga marufuku shughuli za Kituo cha Kiislamu cha Hamburg
Jul 25, 2024 00:58Serikali ya Ujerumani imechukua hatua ya kibaguzi ya kukifunga Kituo cha Kiislamu cha Hamburg na mashirika tanzu nchini humo kutokana na kile ilichodai ni kueneza itikadi kali na idiolojia ya Kiislamu.
-
WHO yabainisha wasiwasi mkubwa juu ya uwezekano wa kutokea mlipuko mkubwa wa polio huko Gaza
Jul 24, 2024 09:28Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa lina wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa kutokea mlipuko mkubwa wa polio huko Ukanda wa Gaza kufuatia kugunduliwa hivi karibuni virusi vya polio kwenye maji taka.
-
Duru mpya ya mazungumzo ya pamoja ya usalama kati ya Marekani na Iraq mjini Washington
Jul 24, 2024 07:44Alina Romanowski, balozi wa Marekani mjini Baghdad, alitangaza siku ya Jumatatu kuhusu kuanza mazungumzo kati ya Marekani na Iraq huko Washington mji mkuu wa Marekani ajenda kuu ikiwa ni "mustakabali wa muungano wa kimataifa."
-
Time: Kwa nini Ufaransa inapiga marufuku vazi la hijabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris?
Jul 24, 2024 06:35Jarida la Marekani la "Time" limeripoti kuwa Ufaransa haitarudi nyuma katika uamuzi wake unaowazuia wanariadha wa Ufaransa wanaovaa vazi la staha la hijabu kushiriki katika Michezo ya Olimpiki itakayoanza mjini Paris Ijumaa ijayo.
-
Japan yawawekea vikwazo walowezi Waisraeli kutokana na jinai dhidi ya Wapalestina
Jul 23, 2024 09:53Japan kwa mara ya kwanza imewawekea vikwazo walowezi wanne Wazayuni Waisraeli kutokana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
-
Pakistan yamtangaza rasmi Netanyahu kuwa ni gaidi, yaitaka Jamii ya Kimataifa nayo pia ifanye hivyo
Jul 23, 2024 03:02Serikali ya Pakistan imetangaza kuwa Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni, ni "gaidi".