Duru mpya ya mazungumzo ya pamoja ya usalama kati ya Marekani na Iraq mjini Washington
(last modified 2024-07-24T11:14:58+00:00 )
Jul 24, 2024 11:14 UTC
  • Duru mpya ya mazungumzo ya pamoja ya usalama kati ya Marekani na Iraq mjini Washington

Alina Romanowski, balozi wa Marekani mjini Baghdad, alitangaza siku ya Jumatatu kuhusu kuanza mazungumzo kati ya Marekani na Iraq huko Washington mji mkuu wa Marekani ajenda kuu ikiwa ni "mustakabali wa muungano wa kimataifa."

Tangu mwaka 2014, takriban wanajeshi 2,500 wa Marekani wamekuwepo nchini Iraq kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daes, na wanajeshi hao wamesambazwa katika vituo vitatu kuu: Ain al-Asad mjini Anbar, Harir mjini Erbil, na Camp Victory jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. 

Kwa miaka mingi wananchi wa Iraq wamekuwa wakitaka kuondolewa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq, kwa sababu kwa upande mmoja,  Marekani inakiuka mamlaka ya kujitawala Iraq, na kwa upande mwingine, sio tu kwamba usalama wa nchi hiyo haujadhaminiwa, bali Marekani iliwashambulia na kuwaua kwa ndege ya isiyokuwa na rubani katika ardhi ya Iraq Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Hashd al-Sha'abi ya Iraq na Luteni Jenerali Qassim Suleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) tarehe 3,2020. Jinai hii ya Marekani ilifuatiwa na kuibuka hasira na ghadhabu kali za wananchi wa Iraq.

Mashahidi Qassem Soleimani na Abu Mahdi Al Muhandis

Mazungumzo kati ya Baghdad na Washington yalianza Februari mwaka huu kwa kupasishwa upunguzaji wa hatua kwa hatua wa idadi ya vikosi vya eti muungano wa kimataifa dhidi ya Daesh na hatimaye kumaliza kazi ya vikosi hivyo, na duru mbili zingine za mazungumzo hayo zilifanyika katika miezi ya Machi na Aprili.

Mohammad Shia al-Sudani, Waziri Mkuu wa Iraq ametangaza kuwa, Kamati Kuu ya Pamoja ya Kijeshi ya Marekani na Iraq imekubali kusitisha kazi ya muungano wa kimataifa kwa mujibu wa jedwali, lakini hakuna maelezo yaliyotangazwa ya mchakato wa kuondoka kwa majeshi ya Marekani. Marekani nayo ambayo ilipanga kuwasilisha ratiba ya kupunguza vikosi vyake nchini Iraq mwezi Juni, ilibadilisha uamuzi wake huo bila ya kutoa maelezo yoyote.

Duru mpya ya mazungumzo ya Baghdad-Washington inafanyika huku msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller alisema siku ya Jumatatu kwamba, wawakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani watashiriki katika mkutano wa usalama wa Iraq mjini Washington. Kulingana naye  ni kuwa, wawakilishi wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani pia wanashiriki katika mkutano huo.

 

kuondolewa kwa vikosi vya muungano wa kimataifa kutoka   Iraq; Utata na changamoto

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alikataa kutoa maoni yake kuhusu kuendelea kuwepo kwa vikosi vya kijeshi vya Marekani nchini Iraq, lakini akasema kwamba, tumetoa ahadi yetu kwa kamati ya juu zaidi ya kijeshi ambayo itaanza kufanya kazi. Kamati hii itafanya kazi kuhusu namna ya kubadilisha hali ya vikosi vya jeshi la Marekani. Kulingana na kiwango cha tishio la Daesh kuna haja ya kuweko uendeshaji wa vikosi na mipango mingine.

Wakati Baghdad inasisitiza juu ya ulazima wa kuhitimishwa operesheni za muungano wa kijeshi wa Marekani nchini Iraq, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa, ni jambo lililo mbali katika mazingira ya sasa ambapo Marekani inajiandaa na uchaguzi wa Rais kuiona ikikubali kutia saini makubaliano ya kuondoka kwa vikosi vyake kutoka Iraq.

Abdul Hossein Al-Zalami, mjumbe wa muungano wa Al-Fat'h nchini Iraq, amesema kuwa, Marekani imo mbioni kufanya uchagauzi, hivyo haiwezi kutia saini makubaliano ya kuondoka kwa vikosi vyake kutoka Iraq na jambo hili katika hali ya hivi sasa haliwezekani. Hapo awali vyombo vya habari vya Iraq viliripoti kuwa, Baghdad iliiarifu Washington kwa maneno kwamba vikosi vya muungano wa kimataifa wa Marekani lazima viondoke Iraq katika kipindi cha miezi minane hadi mwaka mmoja, vinginevyo serikali ya Iraq ingechukua msimamo wa upande mmoja na kutangaza mwisho wa uwepo wa Marekani nchini Iraq kulingana na sheria za Iraq.

Tags