-
Waislamu India wapata ahueni kidogo baada ya chama cha Modi kudhoofika
Jun 07, 2024 08:37Matokeo ya uchaguzi mkuu wa India yanaonyesha kuwa muungano wa Waziri Mkuu Narendra Modi umepata viti vichache sana kuliko ilivyotarajiwa.
-
Russia: Tutaendelea kuwepo Burkina Faso; Wamagharibi wanataka kurejesha ukoloni Afrika
Jun 07, 2024 02:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Ouagadougou, Burkina Faso kwamba madola ya Magharibi yanapigania kurejesha ukoloni barani Afrika na wakati huo huo amesisitiza kwa kusema: "Tutatuma wakufunzi wa Russia ili kuisaidia zaidi kijeshi Burkina Faso."
-
Uhispania yajiunga na kesi ya Afrika Kusini ICJ dhidi ya Israel
Jun 06, 2024 23:15Siku chache baada ya Uhispania kutangaza kulitambua rasmi taifa la Palestina, nchi hiyo ya Ulaya imetuma ombi la kujiunga kwenye kesi ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaotenda jinai dhidi ya binadamu huko Gaza.
-
Mkuu wa NATO: Hatutatuma wanajeshi Ukraine
Jun 06, 2024 23:15Katibu Mkuu wa shirika la kijeshi la nchi za Magharibi NATO amesema muungano huo wa kijeshi wa Wamagharibi hauna mpango wa kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine.
-
Ombi la Russia la kuitishwa kikao cha Baraza la Usalama la UN baada ya Ukraine kupata 'baraka' za kushambulia ardhi ya nchi hiyo
Jun 06, 2024 23:14Russia imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liitishe kikao kujadili kile ilichokiita "mwanga wa kijani" ulioonyeshwa na baadhi ya nchi za Magharibi wa kuipa idhini Ukraine ya kushambulia hadi ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
-
Putin: Marekani ni mfadhili mkuu wa mauaji ya umati yanayoendelea Ghaza
Jun 06, 2024 06:24Katika hotuba yake ya karibuni kabisa, Rais Vladimir Putin wa Russia ameitaja hali ya hivi sasa ya Palestina kuwa ni matokeo ya sera za Marekani na kusema kuwa kinachoendelea Ghaza hivi sasa ni mauaji ya umati.
-
Katibu Mkuu wa UN: Lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani 'linaning’inia'
Jun 06, 2024 03:20Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametahadharisha kuhusu hatari ya wazi ya uwezekano wa kutokea ongezeko la joto juu ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi linaloukabili ulimwengu ikiwa uzalishaji wa hewa chafuzi utaendelea kwa viwango vya sasa.
-
Baraza la Wawakilishi la Marekani lakabiliana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC
Jun 06, 2024 01:31Kufuatia ombi la mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) la kutoa kibali cha kukamatwa viongozi wa utawala haramu wa Israel, Baraza la Wawakilishi la Marekani mnamo Jumanne, Juni 4, liliidhinisha mpango wa kuiwekea vikwazo mahakama hiyo ikiwa ni katika kuitetea Tel Aviv kwa hali na mali.
-
Chama cha BJP cha Modi chapoteza wingi wa viti katika uchaguzi wa India
Jun 05, 2024 07:47Chama cha Bharatiya Janata (BJP) cha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kimepoteza wingi wake wa viti bungeni kitaifa baada ya kupata hasara kubwa katika majimbo muhimu, na kuashiria mabadiliko makubwa katika hali ya kisiasa ambayo imekuwa ikitawala nchi hiyo kwa muongo mmoja uliopita.
-
Slovenia imelitambua rasmi taifa la Palestina
Jun 05, 2024 03:31Bunge la Taifa la Slovenia limepiga kura kuunga mkono kuitambua Palestina kama nchi huru. Hayo yameelezwa na Spika Urska Klakocar Zupancic mbele ya bunge hilo.