Putin: Marekani ni mfadhili mkuu wa mauaji ya umati yanayoendelea Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i112626-putin_marekani_ni_mfadhili_mkuu_wa_mauaji_ya_umati_yanayoendelea_ghaza
Katika hotuba yake ya karibuni kabisa, Rais Vladimir Putin wa Russia ameitaja hali ya hivi sasa ya Palestina kuwa ni matokeo ya sera za Marekani na kusema kuwa kinachoendelea Ghaza hivi sasa ni mauaji ya umati.
(last modified 2024-06-06T06:24:26+00:00 )
Jun 06, 2024 06:24 UTC
  • Putin: Marekani ni mfadhili mkuu wa mauaji ya umati yanayoendelea Ghaza

Katika hotuba yake ya karibuni kabisa, Rais Vladimir Putin wa Russia ameitaja hali ya hivi sasa ya Palestina kuwa ni matokeo ya sera za Marekani na kusema kuwa kinachoendelea Ghaza hivi sasa ni mauaji ya umati.

Rais Vladimir Putin amesema hayo katika mkutano na wakurugenzi wa mashirika makubwa ya habari ya kimataifa huko Saint Petersburg na kusisitiza kuwa, siasa mbovu za Marekani ndiye muhusika mkubwa wa maafa yanayotokea Ghaza hivi sasa. Amesema: "Tunaamini kuwa haya ni matokeo ya siasa za Marekani iliyovuruga utatuzi wa suala la Palestina na kukanya njia zote za kuutatua mgogoro huu tata zaidi duniani. 

Rais wa Russia ametilia mkazo pia wajibu wa nchi nyingine duniani kusaidi jitihada za kuwaondolea mateso wananchi wa Palestina hasa wa Ghaza na kusisitiza kwa kusema: "Tuko tayari kufanya kila kitu kutatua suala hili." Vile vile amesema kuwa, suluhisho pekee la mgogoro wa ukanda huu wa Asia Magharibi ni kuundwa nchi huru ya Palestina na kutambuliwa kimmataifa.

Rais Vladimir Putin wa Russia

 

Matamshi hayo ya Putin ya kwamba Marekani ndiye mfadhili mkuu wa jinai za kuitisha za Israel yamekuja huku taarifa nyingine zikisema kuwa, kiwango cha mabomu iliyodondosha Israel huko Ghaza kimevuka cha Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. 

Taarifa hizo za kuaminika zinasema kuwa, hadi hivi sasa utawala wa Kizayuni wa Israel umedondosha zaidi ya tani 70,000 za mabomu kwenye ardhi ya Ukanda wa Ghaza tangu tarehe 7Oktoba mwaka jana, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi kulinganisha na mabomu yote yaliyodondoshwa kwenye miji ya Dresden, Hamburg, na London kwa pamoja wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.