-
Bajeti ya muda ya US yaidhinisha msaada wa kijeshi kwa Israel, yazuia ufadhili kwa UNRWA
Mar 24, 2024 03:06Bunge la Marekani limepitisha pendekezo la bajeti ya muda ambayo imeidhinisha msaada mpya wa kijeshi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusitisha ufadhili kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) hadi Machi 2025.
-
Wasiwasi wa Marekani kuhusu muungano wa Iran, Russia na China
Mar 23, 2024 22:56Kamanda wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) Jenerali Michael E. Kurilla amebainisha wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa ushirikiano kati ya Iran, China na Russia na kudai kuwa ushirikiano wa nchi hizo utakuwa na"matokeo mabaya ya kimataifa".
-
Washukiwa wanne wakuu wa shambulizi la kigaidi la Moscow wakamatwa, idadi ya wahanga imefika 93
Mar 23, 2024 08:28Ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin, imetangaza habari ya kukamatwa watu 11, wakiwemo wanne waliohusika moja kwa moja katika shambulio lililolenga jumba la tamasha mjini Moscow jana Ijumaa, na kuua makumi ya watu.
-
The Washington Post: Kauli za Kushner kuhusu Gaza ni dalili ya sera ya baadaye ya Trump
Mar 23, 2024 08:26Gazeti la Marekani la The Washington Post limeripoti kuwa muhula wa pili wa Donald Trump, iwapo atashinda uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani, "huenda ukamaanisha uungaji mkono mkubwa zaidi wa Washington kwa watawala wa sasa wa Israel wanaotaka kuwafukuza Wapalestina kutoka Gaza na kulikalia tena kwa mabavu eneo hilo."
-
Mcheza soka Muislamu kufukuzwa timu ya taifa ya Ufaransa kwa sababu ya Swaumu, wadau walaani
Mar 23, 2024 08:23Habari ya kufukuzwa mchezaji Mohamed Diawara kwenye kikosi cha timu ya taifa ya soka ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 19 kutokana na kufunga Swaumu ya Ramadhani na kukataa kutekeleza maagizo ya Shirikisho la Soka la Ufaransa lililowataka makocha wa timu hizo kategoria za chini ya miaka 21 kutomwita mchezaji yeyote aliyeamua kufunga mwezi wa Ramadhani na kukataa kula mchana wa mwezi huu, imezusha mjadala mkubwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii.
-
Russia: Umoja wa Ulaya unahusika na mashambulizi ya kigaidi ya Ukraine dhidi ya Warusi
Mar 23, 2024 08:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova, amesema kuwa mipango ya Umoja wa Ulaya ya kutenga euro bilioni 50 kama msaada wa kifedha na kiuchumi kwa ajili ya Ukraine "haitauokoa utawala wa Kinazi huko Kiev."
-
Kula mweleka njama za Marekani za kuunga mkono mauaji ya kimbari ya Israel kwenye UN
Mar 23, 2024 08:11Azimio lililopendekezwa na Marekani la kuunga mkono mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza limegonga ukuta baada ya kupigiwa kura ya veto na Russia na China ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Wito wa maseneta 19 wa Marekani wa kuundwa taifa huru la Palestina
Mar 22, 2024 22:59Maseneta 19 wa chama cha Democratic wametoa wito wa kuundwa taifa huru la Palestina katika barua yao iliyotumwa kwa Rais wa Marekani, Joe Biden.
-
Russia, China zalipigia turufu azimio la US kuhusu Gaza lenye kuunga mkono Israel
Mar 22, 2024 22:58Azimio la Marekani la kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza linalohusishwa na mpango wa wafungwa na mateka limepingwa na Russia na China katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na msimamo wake wa kuiunga mkono Israel.
-
Majeshi ya India, Msumbiji, Tanzania katika mazoezi ya pamoja Bahari ya Hindi
Mar 22, 2024 22:54Mazoezi ya pamoja kati ya majeshi ya majini ya Msumbiji, Tanzania na India yalianza Alhamisi katika pwani ya Afrika Mashariki katika Bahari ya Hindi.