Mar 23, 2024 11:53 UTC
  • Mcheza soka Muislamu kufukuzwa timu ya taifa ya Ufaransa kwa sababu ya Swaumu, wadau walaani

Habari ya kufukuzwa mchezaji Mohamed Diawara kwenye kikosi cha timu ya taifa ya soka ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 19 kutokana na kufunga Swaumu ya Ramadhani na kukataa kutekeleza maagizo ya Shirikisho la Soka la Ufaransa lililowataka makocha wa timu hizo kategoria za chini ya miaka 21 kutomwita mchezaji yeyote aliyeamua kufunga mwezi wa Ramadhani na kukataa kula mchana wa mwezi huu, imezusha mjadala mkubwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa tovuti ya RMC ya Redio ya Ufaransa, uamuzi wa Shirikisho la Soka la Ufaransa kumtenga Diawara, mchezaji wa Lyon, kutoka kwenye orodha ya timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 19 umechukuliwa kwa sababu ya mchezaji huyo kukataa kula mchana wa Ramadhani na kusisitiza kwamba ataendelea kufunga Swaumu.

Baadhi ya wanaharakati na kurasa za michezo kwenye jukwaa la “X” wanasema kwamba sheria zilizowekwa na Shirikisho la Soka la Ufaransa dhidi ya wachezaji Waislamu hazikuwa za haki.  Mmoja wa wanaharakati hao anasema: “Kinachofanywa na Shirikisho la Soka la Ufaransa hakihusiani kabisa na mpira wa miguu wala jinsi mchezo huo unavyosiiamiwa. Uamuzi huo unawalazimisha wachezaji wa soka kuchagua ama kipenzi chao yaani mpira wa miguu, au dini yao ya Kiislamu!"

Timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa

Baadhi ya wanablogu wameshangazwa na jinsi nchi inayodai kupigania sana kile kinachoitwa “uhuru wa maoni na kujiieleza” inavyoweza kujipinga yenyewe kwenye suala la uhuru wa kuamini.

Inafaa kukumbuka pia kuwa Shirikisho la Soka la Ufaransa mwaka jana liliwaarifu marefa wa mpira wa miguuu uu ya uamuzi wake wa kuzuia kusimamishwa kwa muda mechi ili kuruhusu wachezaji Waislamu kufuturu katika mwezi wa Ramadhani.

Mwandishi wa habari za michezo wa Canada ambaye pia ni wakili, Shireen Ahmed, ameandika kwenye mtandao wa kijamiii wa X kwamba: "Ufaransa inaendelea kuwa bingwa wa mienendo iliyodhidi ya Uislamu kwa uamuzi wake wa sasa kabla ya michezo ya Olimpiki ya Paris."

Tags