May 02, 2024 07:43 UTC
  • Iravani: Madai ya uwongo ya Israel dhidi ya Iran; juhudi za kuupotosha ulimwengu kuhusu jinai za Gaza

Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameyataja madai ya uwongo ya Israel dhidi ya Iran kuwa ni juhudi zenye lengo la kupotosha mazingatio ya walimwengu kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.

Amir Saeed Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amewaandikia barua Mwenyekiti wa Kiduru wa Baraza la Usalama na Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kukadhibisha baadhi ya madai yasiyo na mashiko na ya uwongo ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Iravani ameyataja madai hayo ya utawala wa Kizayuni kuwa yasiyo na msingi zaidi ya kuwa ni jitihada za utawala huo baada ya kukata tamaa kwa lengo kupotosha mazingatio ya jamii ya kimataifa kwa jinai na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo wa kibaguzi dhidi ya wananchi wa Palestina huko Ukanda wa Gaza. 

Mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya raia wa Kipalestina wa Gaza 

Balozi Iravani ameongeza kuwa, madai yasiyo na msingi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran ni jitihada za upotoshaji zenye lengo la kufunika na kuhalalisha mashambulizi na hujuma endelevu za Israel dhidi ya Lebanon na ukiukaji wa kila siku wa sheria za kimataifa, hati ya Umoja wa Mataifa na maazimio nambari 1559 na 1701 ya mwaka 2004 na 2006 ya Baraza la Usalama la UN,  unaotekelezwa na utawala huo.  

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa pia ameashiria namna oparesheni ya Iran ya  Ahadi ya Kweli ya kuiadhibu Israel ilivyotekelekezwa katika fremu ya haki ya kujilinda halali na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kuanzisha vita dhidi ya utawalal wa Israel, na haina nia ya kuendesha vita katika siku zijazo.

Tags