May 02, 2024 11:45 UTC
  • Mahdavi: Iran iko tayari kusafirisha vifaa vya matibabu barani Afrika

Katibu wa Baraza la Sera ya Mauzo ya Nje la Shirika la Chakula na Dawa la Wizara ya Afya ya Iran ametangaza utayarifu wa Iran wa kusafirisha vifaa na suhula za matibabu barani Afrika.

Akizungumzia uwezo wa Iran katika kuzalisha vifaa vya matibabu Asif Mahdavi amesema kuwa, watengenezaji 1,700 wa vifaa vya matibabu wanafanya kazi nchini Iran, hivyo Iran inaweza kuzalisha bidhaa hizo na kusafirisha katika nchi za Afrika.

Mahdavi ameongeza kuwa, vifaa na nyenzo za matibabu zinazotengenezwa na Iran zinasafirishwa kwenda nchi mbalimbali za Asia Magharibi, Asia na hata Ulaya, na uwezekano wa ushirikiano katika uga wa kurahisisha usafirishaji wa dawa barani Afrika tayarii umeshaandaliwa.

Katibu wa Baraza la Sera ya Mauzo ya Nje la Shirika la Chakula na Dawa la Wizara ya Afya ya Iran amesema, wazalishaji wa Iran wanaweza kuzisaidia nchi za Kiafrika katika uga wa kupeleka teknolojia ya utengenezaji wa vifaa na pia kudhamini mapungufu katika uwanja huo.

Sayyid Asif Mahdavi, Katibu wa Baraza la Sera ya Mauzo ya Nje la Shirika la Chakula na Dawa la Wizara ya Afya ya Iran

 

Kwa mujibu wa maafisa wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Kitabibu ya Iran, Jamhuri ya Kiislamu inahesabiwa kuwa miongoni mwa nchi zilizoendelea katika vigezo vingi vya matibabu duniani, kwa namna ambayo inashika nafasi ya 15 katika masuala ya tiba na ya 7 katika masuala ya dawa.

Katika uga wa uwezo na maendeleo ya kitiba na dawa, Iran ni miongoni mwa nchi ambazo zimetambuliwa na asasi za kisayansi na kimataifa katika uga wa tiba.

Tags