May 02, 2024 02:36 UTC
  • Hakan Fidan: Uturuki itaomba kujiunga katika kesi ya mauaji ya kimbari inayoikabili Israel huko ICJ

Hakan Fidan Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema kuwa nchi hiyo itaomba kuwa sehemu ya kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya Israel. Itakumbukwa kuwa serikali ya Afrika Kusini imefungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na mauaji yake ya kimbari huko Gaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amebainisha haya jana katika mkutano na waandishi wa habari  katika mji mkuu wa nchi hiyo Ankara akiwa na mwenzake wa Indonesia, Retno Marsudi.

Katika mazungumzo hayo huko Ankara pamoja na mambo mengine, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki na Indonesia wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusu Palestina na hali ya mambo ya Ukanda wa Gaza. 

Fidan ameongeza kuwa anatumai kuwa kwa mchakato huu uliowasilishwa katika  mahakama ya ICJ mambo yote yatakwenda katika mkondo sahihi. Amesema kwa muda mrefu Uturuki imekuwa ikifanya kila iwezako ili kukubaliwa ombi lake la kujiunga katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Afrika Kusini ambapo utawala wa Kizayuni umetuhumiwa kwa mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. 

Majaji wa Afrika Kusini katika mahakama ya ICJ 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ameongeza kuwa Ankara itaendelea kuwa pamoja na wananchi wa Palestina katika hali zote."

Tags