-
Vyombo vya habari Ulaya vyafichua mpango wa kifisadi wa Rais wa FIFA na wandani wa Trump
Aug 05, 2026 02:38Jarida la The Times limefichua kiasi kikubwa cha fedha ambazo rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino, angeweka mfukoni iwapo mpango wa kuuza Kombe la Dunia ungetekelezwa.
-
Algeria na Italia zakubaliana kuimarisha ushirikiano ili kupambana na uhamiaji haramu
Aug 04, 2026 10:19Algeria na Italia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano dhidi ya uhamiaji haramu na uhalifu wa kuvuka mipaka. Uamuzi huu umefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Mawaziri wa Mambo ya Ndani wan chi mbili hizo huko Roma, Italia.
-
Leo ni Arubaini ya Imam Hussein AS, Waislamu wa Iran waungana na Waislamu wengine kuiadhimisha
Aug 04, 2026 03:14Jumanne ya leo ya tarehe 4 Agosti 2026 inasadifiana na maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS, yaani siku ya 40 tangu Imam Husain AS na wafuasi wake watiifu walipouawa kinyama kwenye jangwa la Karbala mwezi 10 Mfunguo Nne Muharram, mwaka wa 61 Hijria.
-
Ripoti ya Middle East Monitor: Mwisho wa dhana ya Marekani ya 'kutoshindwa'
Aug 03, 2026 02:45Ripoti ya gazeti la Middle East Monitor imesema kuwa, Iran haiwezi kushindwa katika vita, na kwamba hali hiyo ni ukweli ambao Marekani na Israel haziwezi kuubadilisha hata kama watajitahidi kiasi gani.
-
New York Times: Umaskini wakithiri Marekani, pengo la kijamii lazidi kupanuka
Aug 03, 2026 02:43Gazeti la New York Times limeripoti kuongezeka umaskini nchini Marekani na kuongezeka pengo la kijamii miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo.
-
Jenerali wa Marekani: Hatuna vikosi vya kutosha vya kuilinda Israel na makombora ya Iran
Aug 02, 2026 02:49Gazeti la The Washington Post limeandika: Jenerali mmoja mwandamizi wa Marekani barani Ulaya ameionya Pentagon kuwa Jeshi la Wanamaji halina vikosi vya kutosha vya kuweza kuendelea kuilinda Israel na makombora ya masafa marefu.
-
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu utumiaji wa mada zilizopigwa marufuku dhidi ya raia wa Iran
Aug 01, 2026 11:26Maripota wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa taarifa ya pamoja, wakisema kuwa raia 3,375 wa Iran wameuawa katika mashambulizi ya kikatili ya Marekani na Israel (wakiwemo wanawake wapatao 500), na kutoa wito wa kuwajibishwa Marekani na Israel kwa uhalifu wao wa kivita, hasa kuhusu janga la shule ya msingi ya Minab.
-
Meya wa Moscow: Zaidi ya droni 6,000 za Ukraine zililenga mji mkuu wa Russia mwezi Julai
Aug 01, 2026 11:18Zaidi ya ndege zisizo na rubani (droni) 6,000 za Ukraine ziliulenga mji mkuu wa Russia, Moscow mwezi Julai mwaka huu. Haya yameelezwa na, Meya wa Moscow, Sergey Sobyanin.
-
Kwa nini Nguvu ya Marekani Inaelekea Ukingoni?
Aug 01, 2026 06:08Miongo mitatu baada ya operesheni ya "Desert Storm," mtazamo ndani ya duru za kimkakati za Marekani ni kwamba zama za nguvu na utawala usio na mpinzani wa Washington zimefikia ukingoni. Vita na Iran vimethibitisha kuwa mwenendo wa mabadiliko katika uwiano wa nguvu na kupungua kwa uwezo wa Marekani wa kuzuia vitisho (deterrence credibility) ndani ya mfumo wa dunia umeanza kushika kasi.
-
Karibu nusu ya Wamarekani wanataka Netanyahu akamatwe licha ya propaganda za mamilioni ya dola
Jul 31, 2026 03:31Karibu nusu ya Wamarekani wanataka waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akamatwe licha ya propaganda zinazofanywa na utawala huo wa kizayuni ambazo zimeugharimu mamilioni ya dola.