Feb 27, 2024 07:28 UTC
  • Waislamu wakosoa kutoakisiwa mauaji ya makumi msikitini Burkina Faso

Makumi ya waumini wa Kiislamu waliuawa katika shambulizi dhidi ya msikiti nchini Burkina Faso, siku ambayo watu 15 waliuawa pia katika hujuma nyingine dhidi ya kanisa nchini humo.

Hata hivyo vyombo vya habari vya ndani na nje ya Burkina Faso vilichangamkia shambulizi dhidi ya kanisa, huku vikipuuza hujuma dhidi ya msikiti iliyoua idadi kubwa zaidi ya watu.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekosoa undumakuwili huo wa vyombo vya habari hasa vya Magharibi kwa kutoakisi umwagaji damu huo dhidi ya waumini wa Kiislamu nchini Burkina Faso.

Mashuhuda na maafisa usalama nchini humo waliliambia shirika la habari la AFP jana Jumatatu kuwa, watu waliokuwa wamejizatiti kwa silaha Jumapili alfajiri walishambulia msikiti mmoja katika eneo la Natiaboani, na kuuawa makumi ya Waislamu waliokuwa maabadini hapo kwa ajili ya Swala ya Alfajiri.

Habari zaidi zinasema kuwa, kiongozi mashuhuri wa Kiislamu ni miongoni mwa watu waliouawa kwenye shambulizi hilo la Jumapili alfajiri katika eneo la Fada N'Gourma, yapata kilomita 60 kusini mwa mji wa Fada N'Gourma, mashariki mwa Burkina Faso.

Aidha siku hiyo ya Jumapili, watu wasiopungua 15 waliuawa katika shambulizi jingine dhidi ya Katoliki la Katoliki la Dori katika kijiji cha Essakane, kaskazini mashariki mwa Burkina Faso.

Hakuna kundi lilolodai kuhusika na hujuma hizo za Jumapili dhidi ya maeneo hayo mawili ya ibada. Hata hivyo magaidi wakufurishaji wamekuwa wakiteleza mashambulizi kama hayo dhidi ya misikiti na makanisa nchini Burkina Faso. Kwa muongo mmoja sasa, Burkina Faso imekuwa ikikabiliana na machafuko yanayohusishwa na makundi ya kigaidi ya al-Qaeda na Daesh/ISIS.

 

Tags