Apr 30, 2024 11:15 UTC
  • Rais Ruto aitisha kikao maalum cha baraza la mawaziri huku vifo vya mafuriko vikikaribia 170

Rais William Ruto leo ameongeza kikao maalum cha Baraza la Mawaziri kujadili hali ya mafuriko nchini. Issac Mwaura Msemaji wa serikali ya Kenya ameeleza kuwa mafuriko yameuwa karibu watu 170 mwezi ulioita.

Mapema jana watu wasiopungua 45 walithibitika kufariki dunia wakati vijiji vyao viliposombwa na maji karibu na Mai Mahiu, umbali wa karibu kilomita 60 kutoka mji mkuu, Nairobi. Hata hivyo Shirika la Msalama Mwekundu la Kenya limeeleza kuwa waliopoteza maisha kwa mafuriko ni watu 50.

Mafuriko Kenya 

Rais Ruto amesema kuwa serikali za mitaa zimekosoa hatua za  serikali yake za kukabiliana na mafuriko kuwa za mwendo wa kinyonga. Hata hivyo Rais wa Kenya ametetea hatua zinazotekelezwa sasa na serikali yake katika kipindi hiki cha mafuriko. 

Alipoulizwa iwapo Kenya itatangaza mara moja mafuriko kuwa janga la kitaifa, Rais Ruto amesema kuwa kazi yake ya kwanza ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyoathirika yanapata kile yanachohitaji.

Wataalamu wanasema kuwa mvua zaidi zinatazamiwa kunyesha Kenya; kwa hiyo serikali ya nchi hiyo imeamua shule ziendelee kufungwa. Watu zaidi ya 130,000 wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuriko huku familia nyingi zikiwa zimepata hifadhi mashuleni.