Sudan Kusini yakanusha uwepo wa Wanajeshi wa Uganda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i123820-sudan_kusini_yakanusha_uwepo_wa_wanajeshi_wa_uganda
Wizara ya Habari ya Sudan Kusini imekanusha madai ya uwepo wa wanajeshi wa Uganda nchini humo, baada ya kutangazwa kuwa wameingia nchini humo kulinda usalama.
(last modified 2025-03-12T09:09:53+00:00 )
Mar 12, 2025 09:09 UTC
  • Sudan Kusini yakanusha uwepo wa Wanajeshi wa Uganda

Wizara ya Habari ya Sudan Kusini imekanusha madai ya uwepo wa wanajeshi wa Uganda nchini humo, baada ya kutangazwa kuwa wameingia nchini humo kulinda usalama.

Mkuu wa jeshi la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, katika mfululizo wa machapisho kwenye mtandao wa X, alisema kuwa vikosi maalum vya jeshi lao vimeingia Juba kwa ajili ya kuimarisha usalama wa mji huo.

Katika taarifa hiyo kupitia X, Jenerali Kainerugaba alisema "Tutalinda Eneo Zima la Sudan Kusini Kama Ni Nchi Yetu. Sisi, UPDF, tunamtambua tu Rais mmoja wa Sudan Kusini, Salva Kiir. [...] Hatua yoyote dhidi yake ni tangazo la vita dhidi ya Uganda! Wote watakaofanya uhalifu huo watajifunza maana yake,"

Kwa mujibu wa kamanda hiyo wa  Uganda, operesheni iliyopewa jina la "Mlinzi wa Kimya" imeshaanza rasmi nchini Sudan Kusini.

Waziri wa Habari wa Sudan Kusini, Michael Makuei, Eye Radio, kituo cha redio cha ndani ya nchi, kuwa ripoti za kupelekwa kwa wanajeshi wa Uganda si za kweli

 Mvutano umeongezeka katika siku za hivi karibuni nchini Sudan Kusini, tangu serikali ya Rais Salva Kiir iwakamate Mawaziri wawili na maafisa kadhaa waandamizi wa jeshi waliokuwa wakimuunga mkono Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar.