Kutimuliwa mfululizo viongozi Tunisia; kunani?!
Tunisia imeshuhudia mabadiliko ya mfululizo, ya mara kwa mara na ya ghafla katika nafasi ya waziri mkuu tangu Kais Saied aingie madarakani na kushika wadhifa wa urais.
Kwa mujibu wa mwandishi wa televisheni ya Al-Alam, Rais wa Tunisia juzi Ijumaa alimfukuza kazini Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Kamal Madouri, katika hatua iliyochukuliwa ghafla bila ya kutarajiwa. Huyu ni waziri mkuu wa nne ambaye amemfuta kazi tangu ashike kiti cha urais mwaka 2021.
Rais wa Tunisia Kais Saied amemfukuza kazini Waziri Mkuu Kamal Madouri na kumteua Sara Zafarani kuunda baraza jipya la mawaziri.
Rais wa Tunisia, ambaye tarehe 8 Agosti iliyopita alichukua hatua ya ghafla ya kumfuta kazi Waziri Mkuu Ahmed El-Hashani na kumteua Waziri wa Masuala ya Kijamii Kamel El-Madoury kuwa Waziri Mkuu mpya wa Tunisia, sasa amemfukuza kazini Kamel El-Madoury baada ya kushikilia wadhifa huo kwa miezi minane tu.
Kais Saeid amelishutumu baraza la mawaziri la Al-Madouri kuwa ni maficho ya wabadhirifu na sasa amemteua Waziri wa Maendeleo ya Miji Sarah Al-Zafarani kuwa waziri mkuu.
Wataalamu wanaamini kuwa kukosekana njia za kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii kumemfanya Kais Saeid kuendelea kuwafuta kazi mfululizo viongozi wa utawala wake.
Wachambuzi hao wa mambo aidha wanasema kwamba mabadiliko ya mfululizo katika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tunisia katika kipindi cha miaka minne iliyopita ni mbinu ya kisiasa ya Kais Saied ya kuficha matatizo ya kiuchumi na kisiasa ya nchi hiyo yanayotokana na hatua zake za moja kwa moja. Kais Saied, aliyeingia madarakani kidemokrasia mwaka wa 2019, alihodhi madaraka yote ya nchi Julai 25, 2021, na kuwaweka kando wapinzani wake. Katika uchaguzi wa rais wa mwaka jana, alitaka kuunganisha mamlaka yake na kaulimbiu kama vile "vita vya ukombozi," "vita vya kujitawala," na "kuanzishwa jamhuri mpya."