Maelfu ya Wamorocco waandaamana kupinga kutia nanga meli za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i129124
Maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano katika bandari kubwa zaidi ya nchi hiyo huko Tanger Med kaskazini mwa nchi hiyo kupinga kutia nanga meli zilizobeba silaha za Israel.
(last modified 2025-08-04T08:39:12+00:00 )
Aug 04, 2025 07:37 UTC
  • Maelfu ya Wamorocco waandaamana kupinga kutia nanga meli za Israel

Maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano katika bandari kubwa zaidi ya nchi hiyo huko Tanger Med kaskazini mwa nchi hiyo kupinga kutia nanga meli zilizobeba silaha za Israel.

Waandamanaji wanaituhumu serikali ya Morocco kwa kuusaidia utawala wa Israel katika mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kwa kuziruhusu meli hizo kutia nanga katika bandari ya Tanger Med. 

Maandamano hayo yamefuatia mengine yaliyofanywa wiki kadhaa za karibuni ambapo wananchi wa Morocco wameeleza wazi  kukerwa na kile wanachokitaja kuwa ni  ushirikiano wa serikali ya Morocco na utawala wa Israel.

Katika mkondo huo, wafanyakazi wanane wa bandari ya Morocco wamejiuzulu wakipinga msimamo wa serikali. 

Mamlaka za Morocco hadi sasa zimenyamaza kimya kuhusu maandamano hayo, na hazijathibitisha wala kukadhibisha madai ya kuisaidia Israel. 

Hasira imetanda miongoni mwa wananchi wa Morocco kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha viat vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza Oktoba 7 mwaka 2023, huku maandamano yakifanyika mara kwa mara katika miji tofauti, ikiwa ni pamoja na Tangier na Casablanca.