Mazungumzo ya waasi wa M23 na serikali ya Kinshasa katika hatihati
Wakati mapigano yakiripotiwa kuendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumeibuka swali iwapo awamu ya sita ya mazunguumzo kati ya kundi waasi AFC/M23 na serikali ya Kinshasa yatafanyia juma hili jijini Doha kama ilivyotangazwa na mpatanishi nchi ya Qatar au la.
Hadi kufikia sasa bado haijafahamika ikiwa mazungumzo hayo yatafanyika. Baadhi ya ripoti zinasema huenda mazungumzo hayo yakafanyika lakini bado kuna mgawanyiko mkubwa, ambapo pande zote zinatofautiana kuhusu utaratibu wa kusitisha mapigano.
Makubaliano ya amani yaliyopendekezwa kati ya serikali ya Congo na waasi wa M23 wanaodaiwa kuuungwa mkono na Rwanda yanataka kurejesha udhibiti wa serikali katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi.
Serikali ya Kongo na waasi wa M23 kila upande unautuhumu upande wa pili kuwa umekiuka makubaliano ya kusitisha vita.
Mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa M23 yaliongezeka mwezi Januari, wakati waasi hao walipoteka sehemu kubwa ya mashariki yenye utajiri wa madini, ukiwemo mji mkuu wa eneo la Goma.
Maelfu ya watu wameuawa na mamia kwa maelfu ya raia kulazimishwa kuyaacha makazi yao katika vita vinavyoendelea, Umoja wa Mataifa unasema.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) jana lilieleza kuwa waasi wa kundi la M23 limeuwa makumi ya raia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo