Wanamgambo wa RSF washambulia kwa droni maeneo muhimu ya Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i135118-wanamgambo_wa_rsf_washambulia_kwa_droni_maeneo_muhimu_ya_sudan
Wanamgambo wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) wameshambulia vituo muhimu vya Sudan kwa kutumia ndege zisizo na rubani, na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye vituo hivyo.
(last modified 2026-01-04T23:15:00+00:00 )
Jan 04, 2026 23:15 UTC
  • Wanamgambo wa RSF washambulia kwa droni maeneo muhimu ya Sudan

Wanamgambo wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) wameshambulia vituo muhimu vya Sudan kwa kutumia ndege zisizo na rubani, na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye vituo hivyo.

Mashahuda wanasema, ndege zisizo na rubani za wanamgambo wa RSF zililenga vituo vya miundombinu ya mijini na vituo kadhaa muhimu katika majimbo ya Kordofan Kaskazini na White Nile.

Shirika la Umeme la Sudan limetoa taarifa likisema: "Wakati wa shambulio la ndege isiyo na rubani asubuhi ya jana kwenye Kiwanda cha Umeme cha Abyad, makao makuu ya jimbo la Kordofan Kaskazini, kiwanda hicho kiliharibika na jengo lenye mitambo yake likashika moto."

Hayo yanajiri katika hali ambayo, kundi la madakatri wa Sudan limetahadharisha kuhusu maafa tarajiwa ya kiafya na kibinadamu katika mji wa Dalang unaopatikana katika jimbo la Kordofan Kusini. Kundi hilo limesema kuwa mji wa Dalang unaendelea kuzingirwa huku ukikabiliwa na mashambulizi makali ya wanagambo wa RSF.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali umeeleza kuwa mashambulizi makali ya mabomu katika mji wa  Dalang yanajiri  kila siku, na hadi sasa watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa.

Mapigano kati ya jeshi la taifa la Sudan na wanamgambo wa RSF yameongezeka katika miji ya Kordofan katika miezi ya hivi karibuni tangu wapiganaji wa RSF walipoimarisha uwepo wao katika eneo lote jirani la Darfur, na kudhibiti mji wa El Fasher mwezi Oktoba mwaka huu.

Hali hiyo imezidisha Mateso ya watu nchini Sudan katika vita vilivyozuka Aprili 2023 kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Hadi sasa makumi ya maelfu na watu wameuawa na wengine milioni 13 wamekimbia makazi yaO.