Askari jeshi wa UN na raia wauawa na wanamgambo huko Mali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i18949-askari_jeshi_wa_un_na_raia_wauawa_na_wanamgambo_huko_mali
Askari jeshi mmoja wa kulinda amani wa kikosi cha Umoja wa Mataifa na raia wawili wameuawa katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wenye silaha katikati mwa Mali.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Nov 07, 2016 00:48 UTC
  • Askari jeshi wa UN na raia wauawa na wanamgambo huko Mali

Askari jeshi mmoja wa kulinda amani wa kikosi cha Umoja wa Mataifa na raia wawili wameuawa katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wenye silaha katikati mwa Mali.

Watu hao watatu waliuawa jana wakati wakilizuru katika eneo la Mopti katikati mwa Mali kama sehemu ya msafara wa kijeshi. Askari jeshi aliyeuawa alikuwa ni raia wa Togo. Hayo yameelezwa na duru kutoka jeshi la Mali. Wanajeshi wengine kadhaa wa kudumisha amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa pia katika shambulio hilo. 

Mji wa Mopti nchini Mali

Shambulio hilo linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wenye silaha lilitoka jana huko Mopti eneo ambalo si mbali kutoka mji wa Douentza. Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichoko Mali (MINUSMA) kina wanajeshi na polisi zaidi ya 11,000 kutoka mataifa mbalimbali.