Mjumbe wa UN awasili Gambia baada ya Rais Barrow kurejea nchini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24305-mjumbe_wa_un_awasili_gambia_baada_ya_rais_barrow_kurejea_nchini
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Gambia amewasili katika nchi hiyo ya Kiafrika kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa serikali mpya ya Banjul.
(last modified 2025-10-22T13:08:56+00:00 )
Jan 27, 2017 04:39 UTC
  • Mjumbe wa UN awasili Gambia baada ya Rais Barrow kurejea nchini

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Gambia amewasili katika nchi hiyo ya Kiafrika kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa serikali mpya ya Banjul.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric  amesema Mohammed Ibn Chambas ambaye ni mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Gambia aliwasili katika mji mkuu wa nchi hiyo jana Alkhamisi na anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Adama Barrow, Spika wa Bunge la Gambia, wanadiplomasia wa nchi za kigeni na wawakilishi wa jumuiya za kiraia nchini humo.

 Stephane Dujarric ameongeza kuwa, Mohammed Ibn Chambas atajadiliana na viongozi wa Banjul juu ya jinsi ya kukabidhiana kwa amani madaraka nchini Gambia. 

Image Caption

Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelekea Gambia sambamba Rais mpya wa nchi hiyo, Adama Barrow kurejea nchini kwake jana Alkhamisi akitokea nchi jirani ya Senegal, ambako alikimbilia Januari 15, akihofia usalama wake.

Barrow ameomba kikosi cha askari wa nchi za magharibi mwa Afrika kisalie nchini Gambia kwa kipindi cha miezi sita hadi mambo yatakapotengamaa.