Wanigeria waandamana wakimtaka Rais Buhari arejee nchini au ajiuzulu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32846-wanigeria_waandamana_wakimtaka_rais_buhari_arejee_nchini_au_ajiuzulu
Wananchi wa Nigeria wamedanya maandamano wakimtaka Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo anayepata matibabu kwa zaidi ya miezi mitatu sasa mjini London, Uingereza kwa ugonjwa ambao haujawekwa wazi, arejee nchini au ajiuzulu.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Aug 07, 2017 22:36 UTC
  • Wanigeria waandamana wakimtaka Rais Buhari arejee nchini au ajiuzulu

Wananchi wa Nigeria wamedanya maandamano wakimtaka Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo anayepata matibabu kwa zaidi ya miezi mitatu sasa mjini London, Uingereza kwa ugonjwa ambao haujawekwa wazi, arejee nchini au ajiuzulu.

Rais Buhari aliondoka Nigeria tarehe 7 Mei mwaka huu na kuelekea London Uingereza katika kile kilichotajwa kuwa ni ziara yake ya kitiba na alimteuwa Makamu wake Yemi Osinbajo kukaimu nafasi yake. Makumi ya waaandamaji jana waliandamana hadi katika makazi ya Rais huyo huko Abuja wakiwa wamebeba mabango yanayomtaka Buhari arudi nchini. Moja ya mabango hayo yalikuwa na ujumbe usemao: "Anza kazi au jiuzulu, imetosha".

Maandamano ya wananchi wa Nigeria wakimtaka Rais Buhari arejea nchini au ajiuzulu 

Maandamano hayo ya amani yaliitishwa na muungano wa makundi ya kiraia chini ya usimamizi wa mawakala wa usalama. 

Kumekuwa na tetesi mbalimbali kuhusu hali ya kifaya ya Rais wa Nigeria tangu mwezi Juni mwaka jana ambapo kwa mara ya kwanza alielekea London kwa matibabu yaliyotajwa na Ofisi ya Rais kuwa kiongozi huyo amekuwa akisumbuliwa na maambukizo ya sikio yasiyosita. Afya ya kiongozi huyo wa Nigeria imekuwa kadhia muhimu inayojadliwa tangu kuaga dunia Umaru Musa Yar'Adua rais wa zamani wa nchi hiyo mwaka 2010 baada ya kukaa nje kwa matibabu kwa miezi kadhaa.