Wanajeshi wa Nigeria washambulia kambi ya UN katika mji wa Maiduguri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33024-wanajeshi_wa_nigeria_washambulia_kambi_ya_un_katika_mji_wa_maiduguri
Jeshi la Nigeria limefanya shambulio la kushtukiza katika kambi ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambao ni kitovu cha mapigano kati ya jeshi hilo na wanamgambo wa kitakfiri wa kundi la Boko Haram.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 11, 2017 21:53 UTC
  • Wanajeshi wa Nigeria washambulia kambi ya UN katika mji wa Maiduguri

Jeshi la Nigeria limefanya shambulio la kushtukiza katika kambi ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambao ni kitovu cha mapigano kati ya jeshi hilo na wanamgambo wa kitakfiri wa kundi la Boko Haram.

Lengo la shambulio hilo halijajulikana, lakini wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, hatua hiyo ya jeshi la Nigeria huenda ikaathiri uhusiano ambao tayari umekumbwa na mivutano kati ya jeshi hilo, Umoja wa Mataifa na makundi ya misaada yanayotoa huduma za kibinadamu kwa watu walioathiriwa na mgogoro mkubwa uliosababishwa na hujuma za kundi la Boko Haram.

Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, Samantha Newport amesema kuwa askari jeshi wa Nigeria waliingia katika kambi ya wafanyakazi wa huduma za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa iliyoko Maiduguri bila ya kibali.

Amesema askari hao waliingia kambini asubuhi ya jana Ijumaa na kufanya upekuzi kambini hapo na kwamba waliondoka baada ya masaa matatu. Newport amesema kuwa, Umoja wa Mataifa umesikitishwa sana na vitendo kama hivyo ambavyo vinaweza kusababisha madhara kwa operesheni  ya kutoa huduma muhimu kwa mamilioni ya raia wanaohitaji misaada ya kibinadamu huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. 

Rais wa kaskazini mashariki mwa Nigeria waliolazimika kuwa wakimbizi kutokana na hujuma za Boko Haram