EALA kuanza shughuli zake baada ya Kenya kuwateua wawakilishi wake
(last modified Sun, 17 Dec 2017 08:13:36 GMT )
Dec 17, 2017 08:13 UTC
  • EALA kuanza shughuli zake baada ya Kenya kuwateua wawakilishi wake

Bunge la Afrika Mashariki EALA linatazamiwa kurejelea shughuli zake kuanzia kesho Jumatatu baada ya Kenya kuwateua wawakilishi wake katika chombo hicho cha kieneo.

Msemaji wa EALA, Bobi Odiko amesema miongoni mwa ajenda za kwanza kwenye kikao hicho ni kuapishwa kwa wabunge wa bunge hilo lenye makao yake Arusha, Tanzania.

Aidha Spika wa bunge hilo atateuliwa pamoja na wanachama wa kamisheni na tume mbali mbali za bunge hilo la Afrika Mashariki.

Bendera za nchi wanachama wa EAC

Kadhalika bunge hilo la kieneo linasubiriwa na kibarua cha kujadili na kupasisha kuwa sheria, miswada 13.

Itakumbukwa kuwa, Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki walitazamiwa kuapishwa Juni 6 mwaka huu na kuanza vikao vyao mara moja, lakini hilo halikufanyika kwa kuwa Kenya ilichelewa kuwateua wanachama wake 9 wa kuiwakilisha katika taasisi hiyo ya kikanda.

Kenya iliwaidhinisha wanachama wake wa EALA Alkhamisi iliyopita, na hivyo kutamatisha mkwamo huo wa karibu nusu mwaka.

 

Tags