Maandamano Nigeria kulaani kuuawa shahidi mwanachama wa Harakati ya Kiislamu
Wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (INM) wameshiriki katika maandamanao ya amani kulaani kuuawa shahidi mmoja wa wananchama wa ngazi za juu wa harakati hiyo.
Taarifa zinasama wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wameanadamana mbele ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya nchi hiyo katika mji mkuu Abuja ambapo wametoa nara za kutaka uadilifu utekelezwe kwa wale waliomuua shahidi Sheikh Qassim Omar.
Washiriki pia wametaka wale waliohusika na maafa ya Disemba 2015 mjini Zaria wakamatwe na halikadhalika wameitaka serikali imuachilie huru Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Itakumbukwa kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky alitiwa nguvuni na jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 baada ya kuvamia makazi yake katika mji wa Zaria jimboni Kaduna na kufanya mauaji ya umati dhidi ya Waislamu. Taarifa zinasema mamia ya Waislamu waliuawa shahidi katika hujuma hiyo wakiwemo watoto watatu wa Sheikh Zakzaky.
Hata hivyo licha ya mahakama kutoa hukumu ya kutaka kuachiwa huru mwanazuoni huyo, bado vyombo vya usalama vya Nigeria vinaendelea kumshikilia katika korokoro isiyojulikana huku ripoti zikifichua kwamba hali yake ya kiafya ni mbaya.