Mnangagwa: Fedha za Wazimbabwe zilizokuwa zimefichwa nje ya nchi zimerejeshwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i41893-mnangagwa_fedha_za_wazimbabwe_zilizokuwa_zimefichwa_nje_ya_nchi_zimerejeshwa
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema leo kuwa chini ya nusu ya fedha zilizofichwa nje ya nchi na shakhsia na makampuni mbalimbali zimerejeshwa nchini baada ya kufikia ukomo muhula wa siku 90 zilizotolewa na ameonya kuwa wale wote ambao hawajawajibika watashtakiwa.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 19, 2018 12:01 UTC
  •  Mnangagwa: Fedha za Wazimbabwe zilizokuwa zimefichwa nje ya nchi zimerejeshwa

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema leo kuwa chini ya nusu ya fedha zilizofichwa nje ya nchi na shakhsia na makampuni mbalimbali zimerejeshwa nchini baada ya kufikia ukomo muhula wa siku 90 zilizotolewa na ameonya kuwa wale wote ambao hawajawajibika watashtakiwa.

Itakumbukwa kuwa, wakati alipokula kiapo cha urais mwezi Novemba mwaka jana baada ya Rais Robert Mugabe kulazimishwa kujiuzulu kufuatia mapinduzi ya jeshi, Rais Mnangagwa alitangaza msamaha wa miezi mitatu kwa ajili ya kurejesha fedha za umma zilizokuwa zimefichwa nje ya nchi kinyume cha sheria.

Rais wa zamani za Zimbabwe, Robert Mugabe 

Rais mpya wa Zimbabwe amesema kwamba ni kiasi cha dola milioni 591 pekee ambacho kimerejeshwa nchini hadi sasa kati ya jumla ya dola bilioni 1.42 zinazokadiriwa kuhifadhiwa nje ya nchi kinyume cha sheria. 

Ameongeza kuwa fedha hizo zilizotokana na mapato ya uuzaji nje bidhaa, malipo ya bidhaa zinazoingizwa nchini ambayo kamwe hayajawahi kuingizwa katika mahesabu na fedha zilizokuwa zimefichwa katika benki za kigeni katika mazingira yasiyoeleweka.