Amnesty International yakosoa ongezeko la adhabu ya kifo nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i43042-amnesty_international_yakosoa_ongezeko_la_adhabu_ya_kifo_nchini_nigeria
Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limekosoa ongezeko la hukumu za adhabu ya kifo nchini Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 13, 2018 02:57 UTC
  • Amnesty International yakosoa ongezeko la adhabu ya kifo nchini Nigeria

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limekosoa ongezeko la hukumu za adhabu ya kifo nchini Nigeria.

Taarifa ya shirika hilo iliyotolewa jana Alkhamisi sambamba na kulaani ongezeko hilo imesema kuwa, mwaka 2017 pekee watu 621 walihukumiwa adhabu ya kifo kiwango ambacho ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na miaka 2015 na 2016. Vyombo vya mahakama nchini Nigeria viliwahukumu adhabu ya kifo watu 527 mwaka 2016, huku mwaka mmoja kabla, yaani 2015 vikiwahukumu adhabu hiyo hiyo watu 171.

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) 

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Msamaha Duniani, karibu watu 2285 nchini Nigeria wanasubiri kutekelezewa hukumu ya kunyongwa. Chanzo cha kuongezeka hukumu hizo ni aina ya uainishaji makosa yanayopelekea kunyongwa nchini humo. Hii ni kusema kuwa, katika majimbo tofauti ya Nigeria makosa kama vile wizi wa kutumia silaha, mauaji, mahusiano haramu ya kijinsia, mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja na uhaini, ni mambo ambayo yamewekewa adhabu ya kifo nchini Nigeria.