Wafanyakazi wa sekta ya umma Zimbabwe wakataa nyongeza kubwa ya mshahara
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44542-wafanyakazi_wa_sekta_ya_umma_zimbabwe_wakataa_nyongeza_kubwa_ya_mshahara
Wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Zimbabwe wamekataa nyongeza ya mshahara ya asilimia 15 iliyoahidiwa na serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo na wametaka kuzidishwa zaidi ya mara mbili mshahara wa watumishi wa kiwango cha chini.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 16, 2018 03:18 UTC
  • Wafanyakazi wa sekta ya umma Zimbabwe wakataa nyongeza kubwa ya mshahara

Wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Zimbabwe wamekataa nyongeza ya mshahara ya asilimia 15 iliyoahidiwa na serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo na wametaka kuzidishwa zaidi ya mara mbili mshahara wa watumishi wa kiwango cha chini.

Wiki iliyopita serikali ya Zimbabwe ilikubali kuwaongezea polisi, wanajeshi na watumishi wengine nyongeza ya asilimia kumi katika mishahara yao kuanzia mwezi Julai wakati nchi hiyo inapotarajia kuendesha uchaguzi wa mkuu wa kwanza tangu Robert Mugabe ang'atuke madarakani. 

Baraza la Apec ambao ni muungo unaowawakilisha wafanyakazi wote wa serikali umesema kuwa nyongeza hiyo kubwa ya mishahara iliyoahidiwa na serikali bado iko chini ya mstari wa umaskini; kipimo ambacho  hutumiwa kutathmini iwapo mtu anahesabiwa kuwa ni maskini.  Mtumishi wa serikali wa kiwango cha chini kabisa hupata mshahara wa dola 253 kwa mwezi.  Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika tayari imeshatumia zaidi ya asilimia 90 ya bajeti ya taifa kwa ajili ya mishahara na mafao ya uzeeni, hata hivyo Rais Mnangagwa anajaribu kila linalowezekana kuzuia migomo ya wafanyakazi wa sekta ya umma kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo.