Aug 08, 2018 14:41 UTC
  • Tendani Biti
    Tendani Biti

Kiongozi mmoja maarufu wa upinzani ametiwa mbaroni nchini Zimbabwe wakati alipokuwa mbioni kutoroka nje ya nchi.

Tendai Biti, mmoja wa wapinzani wakubwa wa serikali ya Zimbabwe amekamatwa kwa tuhuma za kuchochea machafuko baada ya uchaguzi wa hivi karibuni wa rais ambao wapinzani wameyakataa matokeo yake.

Katika uchaguzi wa kwanza wa rais kufanyika nchini Zimbabwe bila ya Robert Mugabe, Emmerson Mnangagwa, rais wa hivi sasa wa nchi hiyo amefanikiwa kupata ushindi kwa tofauti ndogo tu ya kura dhidi ya mpinzani wake kutoka chama cha MDC.

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe

 

Chama cha upinzani cha MDC kimelalamikia matokeo hayo na kuituhumu serikali kuwa imefanya udanganyifu mkubwa katika matokeo ya kura.

Wafuasi wa chama hicho cha upinzani walifanya fujo tarehe Mosi mwezi huu wa Mei, lakiji jeshi la Zimbabwe liliingilia kati na kuzima machafuko.

Uchaguzi wa kwanza wa rais baada ya miaka 37 ya utawala wa Robert Mugabe ulifanyika nchini Zimbabwe tarehe 30 Julai. Katika uchaguzi huo, Rais Emmerson Mnangagwa alishinda kwa asilimia 50.8 ya kura akifuatiwa na mgombea wa chama cha MDC Nelson Chamisa aliyepata asilimia 44.3 ya kura zote kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo.

Tags