UN: Msaada wa haraka unahitajika kwa waathirika wa baa la njaa Zimbabwe
Msemaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) amesema kuwa shirika hilo linahitajia msaada wa haraka wa zaidi ya tani milioni moja za chakula kwa ajili ya raia walioathiriwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.
Ashley Backstrom amesema kuwa kwa kuzingatia kuendelea hali ya ukame na kupungua uzalishaji wa mazao ya kilimo nchini Zimbabwe; shirika la WFP haliko tayari kutoa misaada ya dharura na kuwadhaminia chakula jumla ya watu milioni moja laki moja elfu 35 na 500 katika kipindi hiki ambapo kuna uhaba mkubwa wa chakula nchini humo. Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umetangaza kuwa unahitaji zaidi ya Euro milioni 61 ili kuweza kutoa misaada haraka kwa raia walioathirika na baa la njaa huko Zimbabwe.
Ripoti rasmi kutoka Zimbabwe inaeleza kuwa karibu watu milioni mbili na laki nne watakabiliwa na uhaba wa chakula kuanzia mwaka huu wa 2018 hadi 2019. Ni miaka kadhaa sasa maeno ya kusini mwa Afrika yanakabiliwa na ukame ambao umesababishwa na athari hasi za mabadiliko ya tabia nchi ya El -Nino.