Kimbunga Idai chaua watu 24 Zimbabwe na kusababisha uharibifu mkubwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i52205-kimbunga_idai_chaua_watu_24_zimbabwe_na_kusababisha_uharibifu_mkubwa
Watu wasiopungua 24 wamepoteza maisha kusini mashairki mwa Zimbabwe huku madaraja yakisombwa na maji baada ya kimbunga Idai kuikumba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
(last modified 2024-06-10T09:25:34+00:00 )
Mar 16, 2019 14:40 UTC
  • Kimbunga Idai chaua watu 24 Zimbabwe na kusababisha uharibifu mkubwa

Watu wasiopungua 24 wamepoteza maisha kusini mashairki mwa Zimbabwe huku madaraja yakisombwa na maji baada ya kimbunga Idai kuikumba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Kimbuka Idai ambacho kimesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa Msumbuji na Malawi, Ijumaa kilifika Zimbabwe na kupelekea umeme na mawasiliano kukatika nchini humo.

Wizara ya Habari ya Zimbabwe imesema aghalabu ya watu 24 waliofarikia ni kutoka Chimanimami Mashariki huku wengine 40 wakitoweka.

Mbunge wa Chimanimami Mashariki Joshua Sacco amesema kimbunga hicho kimesababusha uharibifu sawa na ule uliosababisha na Kimbunga Eline Februari 2000 kusini mwa Zimbabwe.

Sacco amesema huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka huku waokoaji wakiendelea kuwatafuta watu waliotoweka na ambao hatima yao haijulikani.

Kimbunga Idai 

Helikopta za Jeshi la Anga la Zimbabwe zinatekeleza oparesheni za uokoaji lakini kazi hiyo imetatizwa kutokana na upepo mkali.

Kimbunga hicho kimeikumba Zimbabwe nchi ambayo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakuka kutokana na kiangazi ambacho kimeharibu mimea na kupelekea watu milioni 5.3 wahitaji misaada mwaka huu.

Maeneo makubwa ya Msumbiji, Malawi na Afrika Kusini yameathiriwa na mafuriko, ambayo yameuwa watu 126 na kuwafanya wengine wapatao milioni moja kukosa makaazi.