Iran yalaani mashambulio ya silaha nchini Niger
(last modified Sat, 20 Mar 2021 08:22:15 GMT )
Mar 20, 2021 08:22 UTC
  • Iran yalaani mashambulio ya silaha nchini Niger

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani mashambulio yaliyofanywa hivi karibuni na wabeba silaha nchini Niger, ambayo yamepelekea makumi ya watu kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

Akilaani shambulio hilo japo jana usiku, Said Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran imesikitishwa sana na mauaji hayo ambayo yamepelekea makumi ya watu wasio na hatia kupoteza maisha.

Amesema kuwa taifa la Iran linaomboleza na serikali pamoja na watu wa Niger kufutia mauaji hayo ya kusikitisha.

Wanamgambo Niger

Serikali ya Niger ilitangaza siku ya Jumanne kwamba watu waliokuwa wamebeba silaha na waliokuwa wamepanda kwenye pikipiki walitekeleza shambulio la kutisha katika eneo moja lenye machafuko nchini humo na kuua kinyama watu wasiopungua 58.

Wahanga wa shambulio hilo walikuwa wanarejea makwao baada ya kufanya shughuli zao za kila siku katika soko moja la mauzo ya mifugo karibu na mpaka wa nchi hiyo na Mali.

Tags