Tume ya Haki Afrika yaitaka Misri isitishe hukumu ya kifo
(last modified Wed, 10 Nov 2021 14:25:25 GMT )
Nov 10, 2021 14:25 UTC
  • Tume ya Haki Afrika yaitaka Misri isitishe hukumu ya kifo

Kamisheni ya Haki za Binadamu na Watu ya Afrika imeitaka serikali ya Misri itengue huku ya kifo dhidi ya watu wanaotuhumiwa kushiriki maandamano jijini Cairo mwaka 2013.

Shirika la habari la Middle East Eye limeripoti habari hiyo leo Jumatano na kuongeza kuwa, kamisheni hiyo imemuandikia barua Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri, ikimtaka asimamishe hukumu ya kifo dhidi ya wanaharakati 26 walioshiriki maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013.

Baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali halali na ya kidemokrasia ya Muhammad Morsi, Sisi alishika hatamu za utawala nchini Misri kufuatia uchaguzi wa kimaonyesho wa rais uliofanyika mwaka 2014.

Tangu wakati huo hadi sasa na kwa kutegemea uungaji mkono wa Magharibi, rais huyo wa Misri amekuwa akitekeleza sera ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa utawala wake.

Morsi aliyepinduliwa na Sisi mwaka 2013

Solomon Ayele Dersso, Rais wa Kamisheni ya Haki za Binadamu na Watu ya Afrika amemtaka Morsi katika barua hiyo kusimamisha hukumu hizo, huku taasisi hiyo ikiendelea kuchunguza madai ya ukiukaji za haki za binadamu yaliyowasilishwa kwake na Chama cha Uhuru na Haki (FJP) cha harakati ya Ikhwanul Muslimin.

Katika miezi ya karibuni, asasi nyingi za kimataifa na za kutetea haki za binadamu zimetoa indhari kuhusu utendaji wa utawala wa Misri unaoongozwa na Sisi katika masuala ya uhuru wa kijamii na kisiasa na ukiukaji wa haki za binadamu.

Tags