Maneva ya pamoja ya kijeshi kati ya Russia na Misri
(last modified Thu, 02 Dec 2021 12:07:51 GMT )
Dec 02, 2021 12:07 UTC
  • Maneva ya pamoja ya kijeshi kati ya Russia na Misri

Kikosi cha wanajeshi wa meli za kivita za Russia katika bahari Nyeusi kimetangaza kuwa meli za nchi hiyo hivi karibuni zitawasili katika bandari ya Alexandria huko Misri kwa ajili ya kushiriki katika maneva ya pamoja na nchi hiyo.

Ofisi ya habari ya kikosi cha wanajeshi wa meli za kivita za Russia leo imetangaza kuwa, maneva ya pamoja ya kijeshi kati ya Russia na Misri kwa jina la "Daraja la Urafiki" yataanza kesho Ijumaa. Russia imetuma meli tatu katika maneva hiyo nchini Misri moja ikiwa ni nyambizi, meli ya kivita na meli ya misaada pamoja na msimamizi wa Kirussia Admeri Grigorovich.

Misri kwa upande wake imetuma manowari mbili na meli moja ya kurusha makombora katika maneva hayo ya pamoja kati yake na Russia.   

Meli za Urusi zitaongozwa na Admeri Viktor Kuchkazov, Kamanda wa kituo cha wanamaji cha Novorossiysk ambacho kitashiriki maneva hayo ya pamoja yatakayoanza kesho huko Misri. Maneva hayo ya kijeshi yatafanyika upande wa mashariki mwa bahari ya Meditarenia na katika sehemu ya bahari karibu na bandari ya Alexandria na yatadumu hadi tarehe 10 mwezi huu wa Disemba.

Wanamaji wa Russia katika maneva 

 

Tags