Morroco yaigaragaza Uhispania na kujiandikia historia ya Kombe la Dunia
Timu ya taifa ya soka ya Morocco imepata ushindi mkubwa kwa kuwaondoa Uhispania kwa mikwaju ya penalti baada ya kutaka sare ya kutofungana.
Morocco ilipachika wavuni mikwaju mitatu huku Uhispania ikishindwa kufunga hata penalty moja. Matokeo hayo yameifanya Morocco kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yake.
Morocco ni nchi ya nne barani Afrika kufika hatua hii ya mashindano hayo, baada ya Cameroon, Senegal na Ghana.
Morocco ambayo imefuzu katika mzunguko wa 16, zaidi ya miaka 30 baada ya kufikia hatua hii kwa mara ya kwanza mnamo 1986, imefaulu katika michuano ya kombe la dunia mwaka huu. Lakini Simba ya Atlas haikusudii kuishia hapo baada ya kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi lililojumuisha Croatia na Ubelgiji.
Morocco inakuwa taifa la nne la Afrika kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia baada ya Cameroon (1990), Senegal (2002) na Ghana (2010).
Wakati huo huo nje ya uwanja, mamia ya watu walikusanyika na kuimba nyimbo za kitaifa, wakipiga picha za furaha na bila kutaka kuondoka uwanjani. Mechi hiyo ilionekana kama mchezo wa nyumbani kwa Simba wa Atlas huku wafuasi wao ambao ni wengi sana nchini Qatar wakiwazidi mashabiki wa Uhispania.
Katika eneo la Souq Waqif ambalo ni maarufu kwa mashabiki hao kukutana mashabiki wa Morocco, Ureno, Tunisia na nchi nyingine za kiarabu walijaa na kuimba nyimbo na kupiga tarumbeta za kushangilia timu ya Morocco.
Ureno yaweka historia yaipa kipigo Uswisi
Nayo timu ya soka ya taifa ya Ureno imetoa onyo kali baada ya kuiangusha Uswisi kwa mabo 6-1 na kuingia robo fainali kwa kishindo katika uwanja wa Kimataifa wa Lusail Doha.
Mshambuliaji Goncalo Ramos aliyecheza badala ya Christiano Ronaldo ambaye alikuwa na hati hati ya kutokucheza kutokana na mvutano na kocha wake.
Lakini kicha alipoulizwa alisema huo ni mvutano wa ndani na wataumaliza wenyewe. Ila iulitajwa kutokea kutokana na Ronaldo kukasirishwa na kitendo cha kocha wake kumtoa katika mchezo uliopita na yeye hakutaka kutoka. Lakini mbadala wake huyo alionyesha makali yake baada ya kupachika mabao 3. Ramos alifunga bao la kwanza katika dakika ya 17.
Naye beki mkongwe Kepler Laveran de Lima Ferreira maarufu kama Pepe ambaye atafikisha miaka 40 mwezi wa pili aliifungia Ureno bao la pili na hivyo kuweka rekodi ya kuwa mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga bao katika awamu ya mtoano katika historia ya Kombe la Dunia. Mshambuliaji Ramos alifunga tena baada ya kipindi cha mapumziko.
Alikamilisha ‘hat trick’ yake baada ya mlinzi Raphaël Guerreiro kuifungia Ureno bao la nne naye Manuel Akanji akaifungia Uswissi bao la kufutia machozi. Jedwali la Robo fainali limekamilika ambapo ni kama ifuatavyo.