Rais wa Zimbabwe aahidi uchaguzi wa Rais utakuwa huru na wa haki
(last modified Thu, 20 Apr 2023 01:28:29 GMT )
Apr 20, 2023 01:28 UTC
  • Rais wa Zimbabwe aahidi uchaguzi wa Rais utakuwa huru na wa haki

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ameonya dhidi ya sauti za kigeni au za ndani, ikiwa ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali yasiyo ya uaminifu ambayo yanachochea migawanyiko na mifarakano.

Rais wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka 80, ambaye atawania katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu, ametoa wito katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 43 ya uhuru wa nchi hiyo, wa kutojihusisha na vurugu, kabla, wakati na baada ya uchaguzi’.

Bunge la Taifa la Zimbabwe lilipitisha sheria yenye utata mapema mwezi Februari inayobana kwa kiasi kikubwa uhuru wa mashirika yasiyo ya kiserikali, na kuyaweka chini ya udhibiti wa serikali.

"Serikali yangu imechukua hatua kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa huru, wa haki na wa kuaminika", amesema Rais Emmarson Mnangagwa wa Zimbabwe. 

Hii ni katika hali ambayo chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe kinamtuhumu Rais Mnangagwa kuwa kanawakandamiza wapinzani wa kisiasa. Katika wiki za hivi karibuni, mikutano ya upinzani imezuiwa huku viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge wakitiwa nguvuni.

Emmerson Mnangagwa ambaye ameshindwa kuboresha hali ya uchumi iliyodorora kwa miaka ishirini sasa licha ya ahadi alizotoa, analaumiwa na wananchi kwa hali ngumu iliyonayo Zimbabwe. 

Mdodoro wa uchumi Zimbabwe