-
John Kerry na kukanusha ukweli usiopingika
Jul 01, 2023 02:24John Kerry, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani katika utawala wa Barack Obama na ambaye ni mwakilishi maalumu wa Washington katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, amezungumzia kile amekitaja kuwa uvamizi wa kijeshi wa Russia huko Ukraine katika mahojiano na televisheni ya Ufaransa.
-
Ubaguzi wa taaluma nchini Uholanzi kutokana na hofu ya vikwazo vya Marekani
Jun 30, 2023 03:15Kufuatia uamuzi wa Taasisi ya Haki za Binadamu ya Uholanzi kwamba kampuni ya nchi hiyo kwa jina ASML inaruhusiwa kukataa kuwaajiri wafanyakazi wake kwa msingi wa utaifa na uraia wao, kampuni hiyo yenye uhusiano mkubwa wa kibiashara na Marekani, siku ya jumatatu ilitangaza kuridhishwa na uamuzi huo uliotolewa kwa maslahi yake.
-
Mgogoro wa Pakistan na matokeo mabaya ya kuhukumiwa maafisa 15 wa jeshi
Jun 29, 2023 23:57Msemaji wa jeshi la Pakistan, Jenerali Ahmed Sharif Chaudhry amesema kuwa, maafisa 15 wa jeshi hilo wametiwa mbaroni wakihusishwa na machafuko yaliyotokewa baada ya kukamatwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Imran Khan.
-
Vikwazo ni sawa na silaha ya kivita
Jun 29, 2023 03:54Katibu wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa, vikwazo ni jinai kubwa dhidi ya binadamu na kwamba Marekani ndiye mtendaji mkuu wa jinai hiyo kutokana na uraibu wake wa kuziwekea vikwazo nchi nyingine bila ya sababu ya maana.
-
Kioja cha karne; si ubaguzi, bali ni sadfa polisi wa Ufaransa kuua Waislamu na watu weusi tu!
Jun 28, 2023 22:59Jumanne jioni, Juni 27, 2023, polisi wa Ufaransa walimpiga risasi na kumuua kijana mdogo Mfaransa mwenye umri wa miaka 17 tu mwenye asili ya Algeria katika kituo cha ukaguzi huko Marseille. Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron imemchukua muda kuchakachua la kusema hadi jana Jumatano na baada ya kutokea fujo kubwa zilizotokana na hasira kubwa za wananchi. Macron ameishia kusema tu kuwa amesikitishwa na mauaji hayo na kuwataka wananchi wasikarike na watulie.
-
Kuzidi kuporomoka nafasi ya Netanyahu huko Israel
Jun 27, 2023 22:51Matokeo ya uchunguzi wa maoni ya hivi karibuni kabisa uliofanywa na vyombo vya habari vya utawala ghasibu wa Israel yanaonyesha kuwa, mapenzi na uungaji mkono kwa Benjamin Netanyahu unazidi kuporomoka huku vyama tanzu katika serikali yake vikizidi kumuacha mkono.
-
Kuendelea ujenzi wa vitongoji haramu vya Israel licha ya kuweko upinzani mkubwa
Jun 27, 2023 09:24Utawala ghasibu wa Israel umeafiki mpango wa ujenzi wa nyumba mpya 5,623 katika Ukingo wa Magharibi ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa kupora na kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Sababu zilizotolewa na Taliban kuhusu kutoruhusu kusoma wasichana wa Afghanistan
Jun 26, 2023 23:16Zabihullah Mujahid, msemaji wa kundi la Taliban la Afghanistan amesema kuwa, kuzuiwa wasichana nchini humo, kusoma masomo ya zaidi ya darasa la sita ni jambo la dharura kwa hivi sasa hadi pale vitabu vya masomo vitakapofanyiwa marekebisho.
-
Mapatano baina ya Kremlin na kundi la Wagner kwa upatanishi wa Aleksandr Lukashenko
Jun 26, 2023 12:01Hatimaye na katika kipindi cha chini ya siku moja, uasi wa kundi la wanamgambo wa Wagner linaloongozwa na Yevgeny Prigozhin umemalizika kwa upatanishi wa Rais Aleksandr Lukashenko wa Belerus.
-
Kukosoa China vigezo vya kindumakuwili katika kukabiliana na ugaidi
Jun 25, 2023 08:55Zhang Jun, balozi na mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amekosoa vikali vigezo vya kindumakuwili vya Marekani kuhusiana na suala la kukabiliana na ugaidi na kueleza kwamba, ugaidi bado ni changamoto muhimu ambayo inatishia amani na usalama wa kimataifa.