-
Sera ya kigeni ya serikali ya awamu ya 13 ya Iran; uwiano, harakati na busara
Jul 23, 2022 00:08Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, siasa za kigeni za serikali ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeegemezwa kwenye siasa za mambo ya nje zenye uwiano, diplomasia yenye harakati na nguvu pamoja na maingiliano yenye busara.
-
Uturuki yaendelea kukiuka mamlaka ya kujitawala Iraq
Jul 22, 2022 23:49Uturuki kwa mara nyingine imekiuka mamlaka ya kujitawala Iraq kwa kuvamia mikoa ya kaskazini mwa nchi hiyo. Jeshi la Uturuki lilifanya shambulio katika kituo cha utalii katika mkoa wa Zakho ulioko katika eneo la Kurdistan ya Iraq Jumatano, na kuwauwa wanawake na watoto wasiopungua 11.
-
Mafanikio ya mkutano wa Tehran katika matamshi ya Erdoğan
Jul 21, 2022 22:02Kama ilivyotazamiwa, Mkutano wa 7 wa "Dhamana ya Mchakato wa Astana" uliofanyika majuzi mjini Tehran umekuwa na mafanikio makubwa kuhusu masuala yanayohusiana na serikali halali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria na watu wa nchi hiyo.
-
Kiongozi Muadhamu: Matukio ya dunia yanadhihirisha haja ya Iran na Russia kushirikiana zaidi
Jul 21, 2022 04:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika mazungumzo na Rais wa Russia hapa Tehran kwamba: matukio ya dunia yanadhihirisha kuwepo haja kwa Iran na Russia kushirikiana zaidi.
-
Kutuhumiwa India kuwa inaunga mkono makundi ya magaidi yaliyoko Afghanistan
Jul 20, 2022 23:59Balozi wa Pakistan mjini Kabul amesema, India inayaunga mkono makundi ya kigaidi nchini Afghanistan ili kuvuruga amani na usalama ndani ya Pakistan.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu la kulindwa na kuheshimiwa umoja wa ardhi yote ya Syria
Jul 20, 2022 04:03Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kulindwa na kuheshimiwa umoja wa ardhi yote ya Syria na akasema: shambulio lolote la kijeshi linalofanywa kaskazini ya Syria, bila ya shaka litakuwa na madhara kwa Uturuki, Syria na eneo zima na litakuwa na manufaa kwa magaidi.
-
Kukiri wataalamu wa Kizayuni kuwa uwezo wa nyuklia wa Iran hauwezi kuharibiwa kijeshi
Jul 19, 2022 21:47Katika kujibu maneno ya Dakta Kamal Kharrazi Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Iran na Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Sera za Kigeni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mkuu wa Majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel amezungumzia kile amekitaja kuwa tishio la Iran na chaguo la kijeshi na kusema chaguo la kijeshi dhidi ya Iran ni jukumu la kimaadili tu.
-
Tofauti kati ya safari ya Biden na Putin eneo la Asia Magharibi
Jul 19, 2022 04:04Baada ya safari ya Rais Joe Biden wa Marekani katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na Saudi Arabia, Rais Vladimir Putin wa Russia leo yuko safarini nchini Iran. Kuna tofauti za wazi kati ya malengo na ajenda za safari ya Biden na Putin katika eneo la Asia Magharibi. Rais Tayyip Erdoğan wa Uturuki pia yuko safarani nchini Iran kwa lengo la mkutano wa pande tatu wa marais wa Iran, Russia na Uturuki.
-
Kumalizika ziara ya makelele mengi ya Biden Magharibi ya Asia na zawadi makhsusi aliyotunukiwa Bin Salman
Jul 18, 2022 21:37Safari ya Rais Joe Biden wa Marekani Magharibi ya Asia imemalizika katika hali ambayo, matunda muhimu iliyozaa ni kufufuliwa nafasi ya Mohammed Bin Salman katika muundo wa madaraka na satua ndani ya Saudi Arabia na katika eneo.
-
Kukiri Tony Blair kwamba enzi za dunia kuhodhiwa na Magharibi zimefikia tamati
Jul 18, 2022 04:09Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair amekiri kuwa enzi za mamlaka-amri, za dunia kuhodhiwa na kudhibitiwa na Magharibi pekee kisiasa na kiuchumi zinakaribia ukingoni na akaeleza kwamba badala yake dunia inaelekea kwenye mfumo wa kambi mbili kuu au yumkini wa kambi kadhaa zenye nguvu.