-
Kuondolewa vikwazo vya Magharibi, sharti la Moscow la kuuza chakula na mbolea nje ya Russia
May 28, 2022 22:56Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, nchi yake haina tatizo na kuuza nje bidhaa za chakula na mbolea na kuikoa dunia na janga hilo, lakini tatizo ni kwa nchi za Magharibi zilizoiwekea vikwazo Russia na kukwamisha zoezi hilo. Amesema, iwapo nchi za Magharibi zitaondoa vikwazo, Moscow itaweza kuendelea kuuza chakula na mbolea kama zamani.
-
Hatua muhimu mno ya kiistratijia ya Bunge la Iraq; uhusiano wowote na Israel ni uhalifu
May 28, 2022 02:40Juzi Alkhamisi tarehe 26 Mei, 2022, Bunge la Iraq lilipasisha kwa kauli moja sheria ya kutambua kuwa ni uhalifu, hatua yoyote ya kuweka uhusiano wa kawaida baina ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kulaaniwa mauaji ya Waislamu wa Kishia Afghanistan
May 27, 2022 22:54Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa wa hali ya haki za binadamu nchini Afghanistan amelaani mauaji ya Waislamu wa Kishia wa jamii ya Hazara nchini humo; na mbali na kubainisha kwamba mauaji hayo yanayoilenga jamii hiyo yameratibiwa kwa mpangilio maalumu ametahadharisha pia juu ya matokeo mabaya ya hujuma hizo.
-
Utawala wa Kizayuni wa Israel, utawala wa mauaji
May 27, 2022 04:40Gazeti la Marekani la New York Times limeripoti kuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umeitaarifu Marekani kwamba ndio uliohusika na mauaji ya Shahidi Hassan Sayyad Khodaei.
-
Iran yakosoa mitazamo ya upande mmoja na taathira zake hasi kwa utulivu wa eneo na usalama wa kimataifa
May 26, 2022 21:53Awamu ya tatu ya mazungumzo ya kisiasa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Italia ilifanyika siku ya Jumanne mjini Tehran, chini ya uenyekiti wa Ali Bagheri, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kisiasa na Ettore Plato, Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia.
-
Mauaji mapya ya ufyatuaji risasi huko Marekani na radiamali ya pupa ya Biden
May 26, 2022 02:10Katika kisa kingine cha ufyatuaji risasi dhidi ya umati nchini Marekani ambacho kimepelekea kuuawa wanafunzi wengi ya shule ya msingi, Rais Joe Biden wa nchi hiyo kama alivyofanya katika siku za nyuma, ametoa radiamali ya pupa na isiyo ya busara katika uwanja huo.
-
Indhari ya Antonio Guterres kuhusu ukimbizi; Asia Magharibi kitovu cha mgogoro
May 25, 2022 23:23Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali mwenendo wa kulazimika watu wa mataifa mbalimbali kuyakimbia makazi yao na kuutaja ukimbizi kuwa ni mgogoro wa kisiasa.
-
Indhari; hali mbaya kabisa ya uchumi wa dunia kuwahi kushuhudiwa tangu Vita vya Pili vya Dunia
May 25, 2022 03:57Baada ya miaka miwili ya msambao wa maradhi ya Covid-19 pamoja na matokeo mabaya yaliyosababishwa na janga hilo na katika hali ambayo, mataifa mbalimbali yalikuwa katika mkakati wa kuboresha uchumi, kutokea vita vya Ukraine na Russia kumevuruga zaidi hali ya uchumi wa dunia.
-
Uhaba wa chakula duniani na matokeo yake
May 24, 2022 21:46Linda Thomas Greenfield, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, indhari ya uhaba wa chakula duniani inayotokana na vita vya Ukraine na Rusia imefikia katika kiwango cha juu kabisa na mazingira ya akthari ya watu ulimwenguni ya kupata chakula yamezidi kuwa magumu siku baada ya siku.
-
Upeo mpya katika uhusiano wa Iran na Oman kufuatia safari ya Raisi mjini Muscat
May 24, 2022 06:30Kufuatia safari ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Oman, upeo mpya umefunguliwa katika uhusiano na ushirikiano wa nchi hizi mbili.