Hamas yataka watawala wa Israel wahukumiwe
Katika taarifa yake, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetaka viongozi wa utawala wa Kizayuni akiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wahukumiwe katika mahakama za kimataifa.
Harakati ya Hamas ilitangaza Jumanne katika taarifa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Hatua za Kibinadamu: 'Tunawataka wavamizi hao wasitishe mauaji ya halaiki na njaa ya kulazimishwa dhidi ya Wapalestina zaidi ya milioni 2 katika Ukanda wa Gaza na kuruhusu mara moja kuingia katika ukanda huo misaada ya kibinadamu.' Katika taarifa hii, Hamas imeongeza: "Tunaichukulia Marekani kuwa mhusika mkuu wa kuendelea mzingiro wa Ukanda wa Gaza na nvurugaji wa juhudi za misaada." Katika taarifa hiyo, harakati ya Hamas huku ikiitaka jamii ya kimataifa kuwafungulia mashitaka watawala wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu wakiongozwa na mhalifu Netanyahu na udharura wa kukomesha jinai zao, imesisitiza kuwa: "Tunathamini juhudi za makundi ya utoaji misaada ambayo yangali yanafanya kazi licha ya mashambulizi ya mabomu na kulengwa watu kwa makusudi.