Pongezi za Kamati za Muqawama wa Palestina/Yemen yafanyia majaribio kombora jipya dhidi ya Israel
Katika shambulio lake la Ijumaa usiku Yemen ilifanyia majaribio kwa mafanikio kombora jipya dhidi ya adui Mzayuni, jambo ambalo lilizifurahisha sana kamati za muqawama wa Palestina na kuzifanya ziwashukuru watu wa Yemen kwa mafanikio hayo.
Vyombo vya habari vya Palestina vimebainisha kuwa, kombora hilo jipya la Yemen lilisababisha hofu kubwa katika anga ya Tel Aviv na kuwa, kombora hilo liligawanyika katika makombora na vipande kadhaa ambavyo vilisababisha uharibifu mkubwa katika nyumba kadhaa za Wazayuni. Vyombo vya habari vya Palestina vimeongeza: Hili ni kombora jipya la jeshi la Yemen lililojaribiwa dhidi ya Israel usiku wa kuamkia Jumamosi. Kamati za muqawama za Palestina pia zimetangaza katika taarifa yao kwamba, kuendelea mashambulizi ya kiubora yanayofanywa na Wayemen kunaonyesha irada thabiti na isiyotikisika ya wananchi wa Yemen, kisiasa na kijeshi na pia azma yao ya kuendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina huko Gaza.