Nov 05, 2023 09:50 UTC
  • Safari ya ujumbe wa kiuchumi wa Afghanistan nchini Iran

Ujumbe wa kiuchumi wa Afganistan umefanya safari nchini Iran kwa madhumuni ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa pande mbili.

Ujumbe huo wa watu 32, unaoongozwa na Mullah Abdul Ghani, ndugu yake naibu mkuu wa kwanza wa serikali ya Taliban ya Afghanistan, mawaziri wa fedha, uchukuzi, usafiri wa anga na biashara wa nchi hiyo. Safari ya ujumbe huo mjini Tehran inaonyesha nia na irada ya Taliban ya kuanzisha uhusiano wa pande zote na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Iran na Afghanistan zina ushirikiano mkubwa wa kibiashara wenye thamani ya dola bilioni mbili kwa mwaka, ambapo sehemu kubwa ya biashara hiyo sio rasmi na hufanyika kwa njia za magendo, kwa maana kuwa haijumuishwi katika takwimu rasmi za serikali. Kwa hivyo, Iran inatarajia kuwa Taliban itachukua hatua zinazohitajika kwa ajili ya kuzuia biashara ya magendo ya bidhaa na mafuta kutoka Iran.

Akram Arefi, Mtaalamu wa masuala ya kisiasa anasema kuhusu hilo: Afghanistan iko katika hali mbaya ya kiuchumi kwa namna ambayo hivi karibuni duru za kimataifa zimesema uchumi wa nchi hiyo unakaribia kusambaratika. Hii ina maana kwamba uchumi huo unahitajia kuboreshwa na kuimarishwa haraka kwa msaada wa nchi za eneo.

Hata hivyo, kutumiwa uwezo wa bandari ya kistratijia ya Chabahar na kusafirishwa bidhaa za kibiashara kupitia njia ya reli ya Khaf-Herat sio tu kwamba kumeanda uwanja muhimu wa kupanuliwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Iran na Afghanistan, bali pia kumerahisisha uhusiano wa kibiashara kati ya  Afghanistan na masoko ya kimataifa.

Viongozi wa ngazi za juu wa Taliban nchini Iran

Katika hatua iliyojikita katika ujirani mwema na kuimarisha ustaarabu, Iran imetoa fursa kwa Afghanistan kwa lengo la kunufaika na Bahari ya Oman kupitia Bandari ya Kimataifa ya Chabahar na bado imeazimia kuimarisha uwepo wa wafanyabiashara wa Afghanistan katika bandari hiyo. Wakati huo huo, reli ya Khawaf-Herat pia imetoa fursa kwa Afghanistan kunufaika na masoko ya kimataifa kupitia njia ya reli nchini Iran.

Hata hivyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga vikali kuingizwa masuala ya kisiasa katika masuala ya usafiri na uhusiano wa kibiashara na inaamini kuwa nchi jirani zinapaswa kutumia uwezo uliopo ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kwa maufaa ya watu wa eneo.

Amin Farjad, Mtaalamu wa masuala ya kisiasa anasema: Afghanistan ina uwezo mzuri wa kuendeleza ushirikiano na Iran, na inatazamiwa kuwa kutumiwa uwezo uliopo wa pande mbili kutaimarisha zaidi uhusiano kati ya Tehran na Kabul. Lakini kama ujumbe wa kiuchumi wa Taliban umefanya safari mjini Tehran ili kuonyesha radiamali yake kuhusiana na mgogoro unaoendelea hivi sasa kati yake na Pakistan basi haitarajiwi kuwa jambo hilo litakidhi matarajio ya muda mrefu katika uhusiano wa Iran na Afghanistan.

Ujumbe wa Afghanistan nchini Iran
 

Kwa vyovyote vile, Iran inahesabiwa kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afghanistan kati ya nchi jirani za kieneo.

Kwa hivyo, safari ya ujumbe wa kiuchumi wa Afghanistan mjini Tehran, ambayo ni ya aina yake katika miaka miwili iliyopita, inachukuliwa kuwa na umuhimu mkubwa, mradi tu mahusiano hayatakuwa ya upande mmoja na Taliban pia ijitahidi kutekeleza matakwa ya pande mbili hususan katika suala la kutekeleza makubaliano yanayohusu mataifa mawili. Pili ni kwamba mtazamo wa  ujumbe wa kiuchumi wa Taliban nchini Iran usiwe ni wa kitaktiki na wa muda tu unaolenga kujibu hatua ya hivi karibuni ya Pakistan ya kuwafukuza wakimbizi wasiokuwa wa kisheria wa nchi hiyo nchini humo. Ni wazi kuwa siasa za kiujanja za aina hiyo si tu hazitakidhi maslahi ya Afghanistan nchini Pakistan bali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia ambayo inachukua hatua muhimu kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kibiashara na Afghanistan kwa maslahi ya watu wa nchi hiyo, inafahamu vyema mambo yanayoendelea pembeni yake kieneo.

 

Tags