Damu safi ya watu wa Gaza itaharakisha mkondo wa kuangamia Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i107014-damu_safi_ya_watu_wa_gaza_itaharakisha_mkondo_wa_kuangamia_israel
Kamanda mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu Iran anasema utawala haramu wa Israel unamwaga damu ya Wapalestina wasio na hatia ili kufidia "kushindwa kwake kwa fedheha" katika vita vya Gaza, akionya kwamba ukatili huo utaharakisha mkondo wa kuangamia kwa utawala huo.
(last modified 2024-01-10T01:07:49+00:00 )
Jan 10, 2024 01:07 UTC
  • Damu safi ya watu wa Gaza itaharakisha mkondo wa kuangamia Israel

Kamanda mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu Iran anasema utawala haramu wa Israel unamwaga damu ya Wapalestina wasio na hatia ili kufidia "kushindwa kwake kwa fedheha" katika vita vya Gaza, akionya kwamba ukatili huo utaharakisha mkondo wa kuangamia kwa utawala huo.

Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi aliyasema hayo siku ya Jumanne, vita vya siku 95 vya mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, vita ambavyo vimechafua kabisa sura ya Israel duniani.

Kamanda wa Jeshi la Iran amesema: "Chini ya uungwaji mkono wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi, utawala haramu wa Kizayuni unalipiza kisasi kuua watoto, wanawake na raia wasio na silaha na wasio na ulinzi baada ya kupata kipigo cha historia mikononi mwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas."

Aidha amesema  hakuna kitakachofidia kushindwa Israel kwa fedheha na bila  shaka damu iliyotakasika ya watu wa Palestina itaharakisha kuanguka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao pia ni utawala wa kibaguzi.

Watoto wa Gaza waliouawa katika hujuma ya Israel

Israel ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina  kwenye Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba baada ya Hamas kutekeleza operesheni ambayo haijawahi kushuhudiwa dhidi ya utawala huo wa Kizayuni ikiwa ni kulipiza kisasi kwa ukatili wa utawala huo  dhidi ya watu wa Palestina.

Hadi sasa utawala wa Israel imewauwa Wapalestina wasiopungua 23,084 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kuwajeruhi wengine 58,926.

Maelfu zaidi pia wametoweka na wanaodhaniwa wamekufa chini ya vifusi katika Ukanda wa Gaza, ambao umezingirwa kikamilifu na Israel.