Profesa wa Iran; Mvumbuzi bora wa mwaka 2023
Profesa Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif cha Tehran, Iran ameshinda Tuzo Bora kwa jina la (Best Patent Award 2023) ya Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kisayansi na Kiteknolojia ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (COMSTECH).
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kisayansi na Kiteknoljia ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (COMSTECH) imetangaza kuwa Tuzo Bora ya Uvumbuzi kwa mwaka uliopita wa 2023 ilitunukiwa kwa pamoja kwa Dk. Samia Koohi, Profesa Msaidizi wa Kitivo cha Uhandisi wa Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif hapa nchini na kwa Mtafiti kutoka Morocco.
Kamati ya COMSTECH ni moja ya njia za ukuaji na maendeleo ya teknolojia na ushirikiano wa kikanda na kimataifa kati ya nchi mbalimbali.
Kamati ya Kudumu ya Ushirikiano wa Kisayansi na Kiteknolojia ya Jumiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (COMSTECH) iliundwa kwa lengo na ili kutilia mkazo maendeleo ya elimu ya ziada, uwekezaji katika sekta ya utafiti, kutoa kipaumbele kwa masuala ya teknolojia ya habari na kubadilishana tatarifa kati ya nchi za Kiislamu.