Mazungumzo ya Zarif mjini Munich
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i1120-mazungumzo_ya_zarif_mjini_munich
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akiwa mjini Munich amefanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu kimataifa kuhusu matukio ya kieneo na dunia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 13, 2016 03:22 UTC
  • Mazungumzo ya Zarif mjini Munich

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akiwa mjini Munich amefanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu kimataifa kuhusu matukio ya kieneo na dunia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRIB, siku ya Ijumaa, pembezoni mwa Mkutano wa Usalama Munich, Zarif amekutana na Jan Eliasson Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Katika kikao hicho Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisisitiza kuhusu kusitishwa mara moja mauaji ya watu wa Yemen. Zarif pia alisisitiza udharura wa kusitishwa umwagaji damu Syria na kupambana kikamilifu na magaidi wakufurishaji. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema baadhi ya nchi za eneo na zilizoko nje ya eneo zinapaswa kufahamu kuwa, usalama wao hautadhaminiwa kwa kuvuruga usalama wa wengine.

Kwa upande wake Jan Eliasson amesisitiza ulazima wa kurejeshwa amani Mashariki ya Kati na baadhi ya nchi za eneo kuwajibuka kuhusu suala hili.

Aidha pembezoni mwa kikao cha usalama Munich, Zarif alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Georgia ambapo wamejadili masuala ya kieneo, mapambano dhidi ya ugaidi na kumalizwa vita katika nchi za eneo.

Kikao cha Usalama cha Munich kilianza Ijumaa alasiri mjini Munich ambapo kitaendelea hadi Jumapili kwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa kisiasa kutoka sehemu mbali mbali duniani.