Aug 27, 2024 11:59 UTC
  • Iran yaalani hujuma ya kigadi nchini Burkina Faso

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran amelaani shambulio la kigaidi huko Burkina Faso ambapo watu zaidi ya 200 wameuwa.

Nasser Kan'ani amelaani vikali shambuli la kigaidi lililofanyika katika eneo la Barsalogho, umbali wa kilometa 40 kaskazini mwa mji wa kimkakati wa Kaya huko Burkina Faso ambapo mamia ya watu wameuawa na wengine kujeruhiwa.

Burkina Faso na hujuma za kigaidi 

Wanajeshi na raia wa kawaida ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika hujuma hiyo ya kigaidi siku kadhaa zilizopita.  

Wanajeshi na raia wa kawaida 340 wameuawa na kujeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi lililotekelezwa Jumamosi tarehe 24 mwezi huu. 

Kundi la kigaidi lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida limekiri kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi huko Barsalogho nchini Burkina Faso. 

Tags