Rais Pezeshkian: Wazayuni wakithubutu kufanya kosa, watapata jibu kali zaidi la Iran
(last modified Wed, 02 Oct 2024 13:32:35 GMT )
Oct 02, 2024 13:32 UTC
  • Rais Pezeshkian: Wazayuni wakithubutu kufanya kosa, watapata jibu kali zaidi la Iran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba operesheni ya makombora ya jana ya kujivunia ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya Israel kwa mara nyingine tena imethibitisha kwamba ngao ya chuma inayodaiwa Wazayuni ni dhaifu kuliko kioo.

Daktari Masoud Pezeshkian amesema hayo leo katika kikao na baraza lake na mawaziri na kubainisha kwamba, tumethibitisha pia kwamba hatufanyi mzaha na mtu yeyote kuuhusiana na suala heshima, izza na mambo ya kujivunia ya taifa letu.

Rais wa Iran amesisitiza kuwa, kama utawala haramu wa Israel unataka kufanya kkosa jingine, basi utambue kwamba, utapata jibu kali na la kuponda zaidi kutoka kwa Iran.

Rais Pezeshkian amesema, hatua ya kuuawa Ismail Haniya ndani ya ardhi ya Iran ilikuwa ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka na usalama wa taifa la Iran na mataifa ya Magharibi yalikuwa yakiitaka Iran ishikamane na subira na yakaahidi kusitisha mara moja vita katika Ukanda wa Gaza.

Mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya Israel

 

Pezeshkian amesema, licha ya wananchi wa taifa hili kuwa na matarajio ya haki ya jibu dhidi ya unyama na mauaji ya Ismail Hania, na sisi hatukuchukua hatua kwa matumaini kwamba, mauaji ya umati dhidi ya watu wasio na hatia Gaza yatasitishwa, lakini Israel imeendelea kufanya mauaji dhidi ya wanawake na watoto huko Gaza na hata kupanua wigo wa jinai zake mpaka Lebanon.

Aidha Rais wa Iran amesikitishwa na kitendo cha madola yanayodai kutetea haki za binadamu ya kuitaka Iran ishikamane na subira na isilipize kisasi cha mauaji ya Ismail Hania na wakati huo huo yananyamazia kimya jinai za Israel ambazo zimeshika kasi na kushadidi katika siku za hivi karibuni.